MFANO WA MATUNDA YA ELIMU YENYE MANUFAA KWA WEMA WALIOPITA-ALLAH AWARIDHIE-.

• قال عبدالله بن وهب رحمه الله :

Amesema Abdullah bin Wahab – Allah amrehemu-:

” نَذَرتُ أني كُلما اغتبتُ إنساناً أن أصوم يوماً، فأجهدني، فكنتُ أغتابُ وأصوم،

Niliweka nadhiri kwamba mimi kila ninapomsengenya mtu nifunge siku moja, basi likanichosha nikawa nasengenya na nafunga ,

فنويتُ أني كلَّما اغتبتُ إنساناً أن أتصدق بدرهم، فمِن حُبِّ الدَّراهم تركتُ الغيبة “.

basi nikanuia kwamba mimi kila ninapomsengenya mtu nitoe sadaka ya dirham moja (pesa), basi kutokana na kupenda dirham (pesa) nikaacha kusengenya.

• علّق عليه الذهبي بقوله : «هكذا والله كان العلماء، وهذا هو ثمرةُ العلم النافع».

(Maneno haya) aliyawekea maelezo mafupi Adh-habyy kwa kauli yake :

” Ni hivi hivi naapa kwa Allah ndivyo walivyokuwa wanawachuoni,na haya ndio matunda ya elimu yenye manufaa”.

المصدر : سير أعلام النبلاء (٢٢٨/٩).

Maelezo ya mpitiaji:

Katika njia za kuikataza nafsi na maovu ni kuiadhibu pindi inapofanya dhambi mfano mtu akaweka nadhiri kama hii ili kuizuia nafsi yake na maovu ,akasema: Nikifanya dhambi fulani nitatoa sadaqa ya shilingi elfu kumi na tano na hii itakuwa ni sababu ya kujiepusha na uovu huo kwa sababu nafsi inapenda pesa na itajisikia uzito kutoa pesa mara kwa mara na itakuwa ni sababu ya kuacha maovu.

Na pia katika tendo hili la huyu mwema aliyepita tunaona kuwa elimu kwa wema waliopita ilikuwa ikitafutwa kwa ajili ya kuifanyia kazi na haya ndiyo matunda ya elimu yenye manufaa kama alivyoeleza imamu Addhahbiy Asshafiy -Allah amrahamu-.

Mpitiaji : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 16, 1443H ≈ Jan 19, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *