NASAHA FUPI KWA MAADMIN/VIONGOZI WA MAGROUP NA WANAGROUP !

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

Kuna baadhi ya watu hudhania kuwa wingi wa faida zinazorushwa na kuwa na member wengi hulifanya group lake likapambanuka na magroup mengine na linakuwa na athari kubwa na wengine wakawa wanaenda mbio ili wapate member wengi !, na wala hawajui kuwa kurusha faida nyingi za kielimu ni kujizidishia hoja juu yao siku ya kiama kwa sababu elimu ni hoja kwa watu wake siku ya kiama.

• قال الشَّعْبِيُّ- رحمه الله-:

Amesema Assha’abiy- Allah amrahamu-:

ليتني لم أكن علمت من هذا العلم شيئا.

“ (Eee) laiti mimi ningekuwa si mwenye kujua chochote katika hii elimu” .

• قال الذهبي معلقا:

Akasema Addhahbiy- Allah amrahamu- hali ya kuyawekea maelezo mafupi (maneno haya):

قلتُ: لأنه حُجة على العالم، فينبغي أن يعمل به، ويُنبه الجاهل فيأمره وينهاه،

Nikasema (Addhabiy):

Kwa sababu hiyo (elimu) ni hoja juu ya mwanachuoni, basi inatakikana aifanyie kazi na amzindue mjinga na amkataze na kumuamrisha ,

ولأنه مظنة أن لا يخلص فيه، وأن يفتخر به ويماري به، لينال رئاسة ودنيا فانية.

Na kwa sababu hiyo (elimu) hudhaniwa kuwa (mhusika) hatotakasa (nia yake) katika hiyo (elimu) ,na akajifaharisha nayo ,na akafanya mijadala kwa hiyo (elimu) ili apate cheo au dunia yenye kuisha.

المصدر : ٣.٣/٤
MAELEZO :

Na faida zinaporushwa kwa wingi watu hushindwa kusoma na kufanyiwa kazi mfano kukiwa kumerushwa faida nyingi katika group wanagruop wanashindwa kujua faida ipi waifanyie kazi na kuzipinda nafsi zao kwa kuitekeleza .

Tutambue kuwa makusudio si kusambaza faida tu bali makusudio ni kukifanyia kazi kile kinachosambazwa.

Basi faida moja unayoisambaza ikaleta athari katika nyoyo na ikamfanya mtu amuogope Allah na kufanya matendo mema ni bora zaidi kwako kuliko kusambaza faida mia moja na zote zikawa ni hoja juu yetu na hasara juu yetu siku ya kiama.

Mwisho:

Kuifanyia kazi elimu ndilo jambo linalotakikana katika dini ama maneno mengi hayazingatiwi ila yatakapothibitishwa ukweli wake kwa matendo , na kama mtu hakuifanyia kazi elimu yake basi elimu hiyo itamfikisha pabaya mhusika na pia yule atakayeisikia elimu hiyo kwa sababu yule atakayesikia jambo la kielimu kama ni la wajibu basi anawajibika kulitekeleza na kama ni katazo la uharamu basi anawajibika kuliacha.

Kwa hiyo kila member wa group ajue kuwa pindi anaposoma ujumbe kutoka katika group au anaposikiliza audio basi ajue kuwa anatakiwa akifanyie kazi hicho alichokifahamu na hilo ndilo kusudio la elimu .

Na maadmin wa magroup wasimamie magroup yao ikiwezekana waweke kiwango maalumu cha kutuma audio au makala kwa siku ili faida ipatikane.

Na pia nawakumbusha umuhimu wa kufanya matendo kwa ajili ya Allah yaani kwa ikhlaswi ili matendo yetu yawe na athari katika nyoyo za watu kama alivyosema mmoja katika wanafunzi wa Maswahaba -Allah amrahamu- :

الكلمة اذا خرجت من القلب وقعت في القلب واذا خرجت من اللسان لم تجاوز الآذان.

“ Maneno yanapotoka moyoni huingia moyoni (moja kwa moja) na yanapotoka ulimini (pekee) hayavuki masikio”

(البيان والتبيين (٥٩/١)

Maana yake: Unapozungumza maneno kwa ikhlaswi moja kwa moja huwaathiri wale unaowaambia ,lakini unapozungumza bila ya ikhlaswi maneno yako yanaishia masikioni mwao tu !

Tunamuomba Allah ulinzi na salama .

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 26, 1443H ≈ Jan 29, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *