Makala namba (4)
قــال الله تعالــى:-
Amesema Allah aliyetukuka-:
﴿إِنَّ اللهَ يُدَافِعُ عَنِ الَّذِينَ آمَنُوا ۗ إِنَّ اللهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ خَوَّانٍ كَفُورٍ﴾
Hakika Allah huwakinga Wale walioamini .Bila shaka Allah hampendi kila mwenye kufanya hiana, mwenye kukanusha neema.
سورة الحج ٣٨
قــال العلامــة عبــدالرحمــٰن السعــدي رحمه الله:-
Amesema mwanachuoni mkubwa Abdul-Rrahman Assi’idiy -Allah amrahamu-:
هـذا إخــبار ووعـد وبشــارة مــن الله، للذيــن آمنــوا، أن الله يدافـع عـنهم كـل مـكروه،
Hii ni habari na ahadi na ni bishara kutoka kwa Allah kwa wale walioamini kwamba Allah huwakinga kutokana na kila lenye kuchukiza,
ويدفـع عنهـم كـل شــر -بسـبب إيمانـهم- مـن شـر الكـفار، وشـر وسـوسة الشـيطان، وشـرور أنفــسهم، وســيئات أعــمالهم،
Na huwakinga kutokana na kila shari kwa sababu ya imani zao (huwakinga) kutokana na shari za makafiri na wasiwasi wa Shetani na shari za nafsi zao na uovu wa matendo yao,
ويحـمل عنـهم عـند نــزول المـكاره، ما لا يتحــملون، فيخـفف عنـهم غايــة التـخفيـف.
Na huwasaidia pindi yanapotokea yale yanayochukiza (kwao) yale ambayo hawayahimili ,basi (Allah) huwawepesishia mno .
كل مؤمـن لـه مـن هـذه الــمدافعة والفــضيلة بحـسب إيمانــه، فمســتقل ومستــكثر».
Kila muumini atapata hii kinga na ubora kwa kadri ya imani yake basi kuna (yule) anayekingwa sana na anayekingwa kwa uchache (kwa kadri ya imani yake)
“تفســير الســعدي (ص٥٣٩)”
Maelezo ya mwandishi:
Allah huwakinga waumini yaani waja wake wema kutokana na shari mbalimbali lakini ukingwaji huu mtu hukingwa kwa kadri ya imani aliyokuwa nayo, na kinga hii huwaenea waumini wote duniani na wala haiwahusu waislamu maalumu lakini sharti ni kusifika na imani kama alivyosema ibn Taimiyyah-Allah amrahamu -baada ya kunukuu hiyo aya kisha akasema:
فَـهوَ تَـبَاركَ وَ تَـعالَىٰ يـدَافِعُ عَـنِ ٱلْمُـؤْمِنينَ حَـيثُ كَـانُوا ، فَاللَّـهُ هُـوَ ٱلـدَّافِع ، وَ ٱلسَّـبَب هُـوَ ٱلْإِيمَـان»
Basi yeye (Allah) -aliyezidi heri na aliyetukuka -huwakinga waumini popote walipo ,Allah pekee ndiye mkingaji ,na sababu (ya kukingwa) ni imani.
“مجمــوع الفتـــاوى صـ ٢٣٠”
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo kumi 13, 1443H ≈ Feb 14, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•