FAIDA KUTOKA KATIKA QURAN

makala namba (5)

قال_تعالى:

Amesema (Allah) aliyetukuk-:

{ ۗ وَمَن يُؤْمِنۢ بِٱللَّهِ يَهْدِ قَلْبَهُۥ ۚ }

{ Na yeyote mwenye kumuamini Allah huuongoza moyo wake}

قال ابن عباس رضي الله عنه:

Amesema ibn Abbas -Allah amridhie-:

«يهدي قلبه لليقين، فيعلم أنَّ ماأصابه لم يكن ليخطئه، وما أخطأه لم يكن ليصيبه».

Huuongoza moyo wake kwa kuwa na yakini akajua kuwa yale yaliyompata hayakuwa yamkose ,na yale yaliyomkosa hayakuwa yampate .

تفسير_الطَّبري (٤٢١/٢٣)

Maelezo ya muandishi:

Kiumbe hawezi kujikinga na shari mbalimbali na yale anayoyachukia kwa uhodari wake na akili yake na bila shaka anachotakiwa ni kutekeleza sababu mbalimbali za kujikinga lakini ajue kuwa alilolikadiria Allah juu yake lazima limpate ,kama yalivyothibiti maneno ya mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- pindi alipokuwa akimfundisha ibn Abbas-Allah amridhie-

واعلَم أنَّ ما أصابَكَ لم يكُن ليُخطِئَك وما أخطأكَ لم يكُن ليُصيبَكَ ، …

Na tambua kuwa lile lililokupata halikuwa likukose na lililokukosa halikuwa likupate…

أخرجه أحمد.

Ufafanuzi:

Na pindi utakapotambua hili basi hakuna linalowajibika juu yako pindi unapopatwa na mtihani isipokuwa ni kusubiri na kutaraji malipo kutoka kwa Allah.

Na kama utaamini kuwa huu mtihani uliokupata ni kadari ya Allah na ndani yake kuna uadilifu wa Allah na hekima yake iliyotimia basi Allah atakuongoza kwa kukupa taufiki ya kuwa na subira na kujisalimisha kwake.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo kumi 13, 1443H ≈ Feb 14, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *