TAMBUA GONJWA LAKO UTAMBUE TIBA YAKE !

▫️قال ابن القيم رحمه الله:

amesema ibn l-Qayyim-Allah amrahamu-:

«المريض الذى يشكو وجع البطن مثلا اذا استعمل دواء ذلك الداء انتفع به، واذا استعمل دواء وجع الرأس لم يصادف داءه.

Mgonjwa ambaye anaugulia maumivu ya tumbo mfano (huyu) akitumia dawa ya hayo maradhi atanufaika nayo ,na pindi atakapotumia dawa ya maumivu ya kichwa (hiyo dawa) haitoafikiana na maradhi yake.

💥 فالشح المطاع مثلا من المهلكات، ولا يزيله صيام مائة عام، ولا قيام ليلها.

Basi mfano ubahili wenye kutiiwa ni katika vyenye kuangamiza hauondoshwi na funga ya miaka 100 na wala kusimama usiku wake

⚠️وكذلك داء اتباع الهوى والاعجاب بالنفس لا يلائمه كثرة قراءة القرآن

Na vilevile gonjwa la kufuata matamanio na kujiona (tiba yake) hainasibiani na wingi wa kusoma quran.

واستفراغ الوسع في العلم والذكر والزهد، وانما يزيله إخراجه من القلب بضده».

Na (wala tiba yake si) kutoa juhudi kubwa katika kutafuta elimu na kumtaja Allah na kuipa nyongo dunia, na hakika si vinginevyo (maradhi) hayo huondolewa kwa kuyatoa moyoni kwa (kuweka) yale yaliyokuwa kinyume na hayo.

📚 عدة الصابرين (ص: ٢١٨).

Maelezo ya mfasiri:

Kila maradhi yana tiba yake sawa sawa yawe yanayoonekana kama homa,kifua,mafua n.k , kama alivyosema mtume-swala na salamu za Allah zimfikie-:

ما أنْزَلَ اللَّهُ داءً إلَّا أنْزَلَ له شِفاءً.

” Allah hakuteremsha maradhi isipokuwa ameyateremshia tiba “

رواه البخاري

na pia maradhi ya kimaana kama :husuda, kiburi, kujiona, n.k .
sheikh -Allah amrahamu-ametoa mfano wa mtu anayeugua maradhi ya tumbo akitumia dawa ya kichwa bila shaka hiyo dawa haitoafikiana na maradhi hayo, kisha akatoa mfano wa maradhi ya kimaana akasema : Mtu ambaye ana maradhi ya ubahili akawa hatoi haki za mali zake kama zaka, kuilisha familia , sadaka au akawa bahili katika kuwafundisha watu elimu aliyokuwa nayo basi bila shaka maradhi haya hayaondoshwi na ibada ya funga hata kama atafunga miaka mia moja na akasimama usiku wake kwa ibada bali anachotakiwa ni kuiondoa tabia hii ya ubahili moyoni mwake na kujilazimisha na tabia ya kutoa na ukarimu.

Vilevile mwenye tabia ya kufuata matamanio ya nafsi yake kwa kumuasi Allah na kujiona, pia mtu wa aina hii akitaka kupambana na tabia hizi chafu anachotakiwa ni kuziondoa kwanza katika moyo wake na kujipamba na tabia mzuri ambazo ni kinyume na hizi ama lau akakithirisha kusoma qurani pekee na akajitahidi kusoma elimu ya kisheria na kumtaja Allah na kuipa nyongo dunia,akidumu na ibada hizi zote bila ya kuziondoa tabia hizi moyoni mwake bila shaka ataendelea kubakia na maradhi yake hayo!

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo kumi 22, 1443H ≈ Feb 23, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *