YANAYOHUSIANA NA FUNGA YA RAMADHANI (NO. 7)
تناول الدواء بعد الفجر!
☞ Kunywa dawa baada ya al-fajiri!
السؤال:
Swali: 📂
تناولت دوائي بعد الفجر في رمضان وقضيت ذلك اليوم فهل علي كفارة ؟
Nimekunywa dawa yangu baada ya al-fajiri katika (mwezi wa) Ramadhani na nikailipa siku hiyo basi je, nawajibika kutoa kafara ?
الجواب:
Jawabu: 📚
لا، الكفارة إنما تجب بالجماع في نهار رمضان،
Hapana, (kutoa) kafara hakika si vinginevyo kunawajibika kwa kufanya tendo la ndoa katika mchana wa Ramadhani,
أما الإفطار بغير الجماع،
Ama kufungulia bila ya tendo la ndoa,
فهو يوجب القضاء فقط.
Basi hilo linawajibisha kulipa tu (bila ya kafara).
📥 المصدر:
Chanzo: (link ya kupata fatwa ya Sheikh hii hapa): 👇🏽
Maelezo ya mfasiri:
Unaposikia adhana ya swala ya al-fajiri hauruhusiwi kufanya tendo la ndoa wala kula wala kunywa na hata kama una chakula kinywani au kinywaji basi unatakiwa ukiteme na kama ukila au ukinywa baada ya kuingia al-fajiri ya kweli basi siku hiyo utawajibika kujizuia na utawajibika kuja kuilipa baada ya Ramadhani,ama kafara hiyo hutolewa na yule aliyefanya tendo la ndoa baada ya kuanza funga yaani baada ya al-fajir na wala si yule aliyeiharibu funga yake kwa mengineyo.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shabani 20, 1443H ≈ Mar 23, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•