لِلشَّــيْخ العَلّامـَـة عَـبْدُ العَزِيـز آل الشَّـيخ – حَـفظهُ الله-:
(Jibu) la Sheikh mwanachuoni mkubwa Abdul – Aziz Aalu Sheikh – Allah amhifadhi:
السُّـؤَالُ:
Swali:
تقضي المرأة المسلمة غالبا كثيرا من وقتها في المطبخ مشغولة بإعداد الأنواع المختلفة من الأطعمة، فيفوت عليها اغتنام أوقات شهر رمضان، فهل من توجيه للمرأة المسلمة؟
Mwanamke wa kiislamu mara nyingi humaliza muda wake jikoni kuandaa aina mbalimbali za vyakula na hupitwa na kutumia fursa ya wakati wa mwezi wa Ramadhani, je kuna muongozo (wowote) kwa mwanamke wa kiislamu?
الجَوَابُ:
Jawabu:
خدمتها في بيتها عبادة لله، وقيامها بواجب بيتها وأولادها عبادة لله، فهي في عبادة إن شاء الله، وعليها أن تغتنم وقتا لذكر الله، وذكر الله ولو عند إصلاح الطعام جائز والحمد لله.
(ile) huduma anayoifanya nyumbani kwake (huko pia) ni kumuabudia Allah – Allah akitaka – na ni juu yake kutumia fursa (ya) wakati kwa kumtaja Allah na kumtaja Allah japo kuwa (utakuwa) wakati wa kuandaa chakula kuna ruhusiwa (kumtaja Allah) na sifa zote ni za Allah.
📝المصــدَرُ:
Chanzo: http://cutt.us/SQ0C
Maelezo:
Mwanamke wa kiislamu pindi anapoandaa chakula kwa ajili ya familia yake au wafungaji atambue kuwa yupo katika ibada katika mwezi huu wa Ramadhani lakini anatakiwa pindi anapofanya kazi hizo ataraji malipo kutoka kwa Allah, afanye kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah, na pia kazi hizo za jikoni zisimfanye aghafilike na kumtaja Allah, bali awe anapika huku akimtaja Allah kwa tasbih na tahmid na tahlil na nyiradi nyinginezo.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Imerudiwa kutumwa Ramadhani 3, 1443H ≈ Apr 4, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•