Makala namba (12)
قال الله تعالى :
Amesema Allah aliyetukuka-:
﴿ وَأَسْبَغَ عَلَيْكُمْ نِعَمَهُ ظَاهِرَةً وَبَاطِنَةً ﴾
{ Na akakuenezeeni neema zake, za dhaahiri na za siri }
سورة لقمان ٢٠
قال ابن عباس رضي الله عنهما :
Amesema ibn Abbas -Allah awaridhie :
النعمة الظاهرة : الإسلام والقرآن ، والباطنة : ما ستر عليك من الذنوب ولم يعجل عليك بالنقمة .
Neema za dhaahiri :Uislamu na Quran, na za siri :Ni yale aliyoyastiri kwako katika madhambi na hakukuharakishia adhabu.
معالم التنزيل (٢٩۱/٦)
Maelezo ya mfasiri :
Hakuna neema kubwa zaidi ya uislamu na makusudio ya uislamu hapa ni ule uislamu ambao alioteremshiwa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie – na neema ya pili katika neema za dhaahiri ni Quran ambayo ni kitabu cha Allah na maneno yake , na aina ya pili ya neema ni neema ya siri ambayo Allah -aliyetukuka- ametuneemesha na maana ya neema hii ni kile kitendo cha Allah kutustiri kwa madhambi tunayoyafanya na lau yangekuwa madhambi yetu yanadhihiri basi tungekimbiana kama alivyosema Al-qahtwaniy -Allah amrahamu-:
والله لو علِموا قبيح سريرتي
= لأبى السلامَ عليّ من يلقاني
Naapa kwa Allah lau (watu) wangejua ubaya wa undani wangu##
Basi angekataa kunitolea salamu yule aliyekutana na mimi.
Na bila ya upole wa Allah na kutustiri kwake kwa madhambi tuliyokuwa nayo asingebakia yeyote katika hii ardhi,kama alivyosema Allah -aliyetukuka -:
وَلَوْ يُؤَاخِذُ اللَّهُ النَّاسَ بِمَا كَسَبُوا مَا تَرَكَ عَلَىٰ ظَهْرِهَا مِن دَابَّةٍ وَلَٰكِن يُؤَخِّرُهُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۖ
Na kama Allah agaliwaadhibu watu kwa sababu ya yale waliyoyachuma, asingaliacha juu ya ardhi (watu wote na) hata mnyama mmoja.Lakini yeye anawachelewesha mpaka (ufike huo) muda (maalumu) uliowekwa.
فاطر ٤٥
Tunamuomba Allah atusamehe madhambi yetu na atusitiri.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shawwal 5, 1443H ≈ May 6, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•