WENGI HAWALIFAHAMU HILI!

🔺قال ابن القيم رحمه الله:

Amesema ibn l-Qayyim-Allah amrahamu -:

«أعمال القلوب في الثواب والعقاب كأعمال الجوارح.

Matendo ya nyoyo katika thawabu na adhabu ni kama matendo ya viungo.

• ولهذا يثاب على الحب والبغض والموالاة والمعاداة في الله، وعلى التوكل والرضى والعزم على الطاعة،

Na kwa ajili hii (muislamu) hulipwa juu ya kupenda na kuchukia,na kupendana/ kunusuriana ,na kufanyiana uadui kwa ajili ya Allah na (hulipwa) juu ya kutegemea na kuridhia na kuazimia twaa (ibada),

ويعاقب على الكبر والحسد والعجب والشك والرياء وظن السوء بالأبرياء».

Na huadhibiwa juu ya kiburi na husuda na kujiona na shaka na kujionesha na kuwadhania vibaya walioepukana na makosa.

📚 زاد المعاد جـ ٥ (صـ ٢٨٨).

Maelezo ya mfasiri :

Usidhani kuwa matendo unayoandikiwa thawabu na utakayoadhibiwa ni yale unayoyafanya kwa viungo vyako tu bali hata matendo yanyoyo pia mtu atalipwa na kuadhibiwa mfano wa matendo hayo ni haya :

1- Kupenda : Ukimpenda muislamu kwa ajili ya Allah tambua kuwa hiyo ni ibada .

2-Kuchukia :Kuwachukia Washirikina na makafiri ni katika ibada, na kuwachukia wazushi katika dini.

3- Kupendana na kuteteana kwa ajili ya Allah, na pia kufanyiana uadui kwa ajili ya Allah ni ibada, lakini hili linavidhibiti vyake kama walivyoeleza wanavyuoni.

4- Kumtegemea Allah : Hii ni ibada kubwa katika ibada za nyoyo

5- Kuridhia kadiri za Allah pia ni katika daraja kubwa za ibada.

6 -Kuazimia juu ya kufanya ibada : Yaani unapoazimia moyoni kuwa utafanya ibada hata unaandikiwa thawabu hata kama hujaifanya.

Haya ambayo sheikh ameyataja ni miongoni mwa matendo ya nyoyo ambayo muislamu huandikiwa thawabu .

Na pia kuna madhambi ambayo hufanywa katika moyo ambayo mja huandikiwa madhambi na katika hayo ni haya :

1- Kiburi:Na kiburi amekieleza Mtume – swala na salamu zimfikie -kuwa ni kuikataa haki na kuwadharau watu.

2- Husuda : Ni gonjwa la mtu kuchukia neema ambayo Allah amemruzuku mwenzake.

3-Kujiona :Ni gonjwa linaloshirikiana na kiburi.

4- Shaka :Na mtu akiwa na shaka na msingi katika misingi ya dini bila shaka anatoka katika uislamu mfano mtu akawa na shaka na uwepo wa kiama n.k .

5- Kujionesha :Na huku kunaporomosha lile tendo ambalo limefanywa kwa ajili ya kujionesha.

6- Kuwadhania vibaya watu walioepukana na makosa :Haifai kuwadhania vibaya watu ila kukiwa na dalili inayopelekea kumdhania mtu vibaya , kama alivyosema Allah -aliyetukuka -:

إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ

Hakika baadhi ya dhana ni dhambi.

الحجرات ١٢

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo Mosi 6, 1443H ≈ May 7, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *