▪️قال الشيخ عبدالرزاق_البدر حفظه الله:
Amesema sheikh Abdul-Rrazzaq Al-Badr -Allah amuhifadhi -:
وقوله صلى الله عليه وسلم :
(( اللّهمَّ استر عوراتي ))
Na kauli yake (Mtume) – swala na salamu za Allah zimfikie-:
“Ewe Allah zistiri aibu zangu “
أي: عيوبي وخَلَلي وتقصيري وكلُّ ما يسوءُني كشفه،
Maana yake : (Zistiri) aibu zangu na makosa yangu na mapungufu yangu na(ukistiri) kila ambacho
kinanifanya nijisikie vibaya kudhihiri kwake,
ويدخل في ذلك الحفظ من انكشاف العورة، وهي في الرَّجل ما بين السرة إلى الركبة، وفي المرأة جَميع بدنها ،
Na linaingia katika hilo :Kuhifadhiwa kutokana na kudhihiri uchi ,na huo (uchi) kwa mwanamume ni lile (eneo) la baina ya kitovu mpaka magotini na kwa mwanamke ni mwili wake wote,
وحريٌّ بالمرأة أن تُحافظ على هذا الدعاء، ولا سيما في هذا الزمان الذي كَثُر فيه في أنحاء العالم تَهَتُّك النساء وعدم عنايتهن بالسِّتر والحجاب،
Na inatakikana kwa mwanamke adumu na dua hii na haswa katika zama hizi ambazo kumekithiri ndani yake katika pande (mbalimbali) za ulimwengu kuwafedhehesha wanawake na kutowatilia umuhimu kwa stara na hijabu,
فتلك تُبدي ساعدَها، والأخرى تَكشف ساقها، وثالثةٌ تُبدي صَدرَها ونحرَها، وأخريات يفعلن ما هو أشد وأقبح من ذلك ،
Basi (utaona) yule anadhihirisha mkono wake na mwingine anadhihirisha ugoko wake na mwingine anadhihirisha kifua chake na shingo yake ,na wengine wanayafanya yale ambayo ni mazito na mabaya zaidi kuliko hayo,
بينما المسلمة الصيِّنة العفيفة تتجنَّب ذلك كلَّه،
Muda ambao muislamu wa kike mwenye kujihifadhi mwenye kujiepusha na machafu (yeye) hujiepusha na yote hayo.
وهي تسأل الله دائما وأبدا أن يحفظها من الفتن، وأن يمنَّ عليها بسَتْرِ عورَتِها .
Na yeye daima na siku zote humuomba Allah amuhifadhi na fitna na amneemeshe (neema) ya kuustiri utupu wake.
📚 فقه الأدعية والأذكار : (32/3) ———————————–
Maelezo ya mfasiri :
Hii ni sehemu ya dua ambayo Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -alikuwa haiachi kuisoma siku zote pindi anapoingia asubuhi na pindi anapoingia jioni kama alivyoeleza ibn Omar -Allah amridhie yeye na baba yake – na dua yenyewe kwa ukamilifu wake ni hii :
- اللَّهمَّ إنِّي أسألُكَ العفوَ والعافيةَ ، في الدُّنيا والآخرةِ ، اللَّهمَّ إنِّي أسألُكَ العفوَ والعافيةَ ، في دِيني و دُنيايَ ، وأهلي ومالي ، اللَّهمَّ استُرْ عَوراتي ، و آمِنْ رَوعاتِي ، اللَّهمَّ احفَظْني من بينِ يديَّ ، ومن خلفي ، وعن يميني ، وعن شمالي ، ومن فَوقِي ، وأعوذُ بعظمتِكَ أن أُغْتَالَ مِن تحتي.
Imepokewa na Abuu Dawd na wengineo.
Na katika yale ambayo mtume alikuwa akiyaomba na anatufundisha sisi pia tumuombe Allah ni kumuomba Allah azistiri aibu zetu, makosa yetu, mapungufu yetu na azistiri tupu zetu zisionekane na kudhihiri kwa watu, na sheikh -Allah amuhifadhi -akaeleza kuwa mwanamke wa kiislamu anatakiwa zaidi adumu na dua hii ya kumuomba Allah amuhifadhi ,auhifadhi mwili wake, na akasema kuwa sisi tupo katika zama ambazo watu hawatilii umuhimu kumuhifadhi mwanamke na kumvesha hijabu bali watu humdhalilisha mwanamke kama tunavyoona mwanamke anavyotumika sehemu mbalimbali katika matangazo ya biashara! na kivutio cha wateja!
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo mosi 10, 1443H ≈ May 11, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•