HIZI NDIZO HATUA ANAZOPITIA BINADAMU !

قال الشيخ العلامة ابن عثيمين رحمه الله تعالى:

Amesema sheikh mwanachuoni mkubwa ibn Uthaimin -Allah aliyetukuka amrahamu -:

والإنسان له خمس مراحل :

Mwanadamu ana hatua tano (anazopitia) :

مرحلة العدم
ثم الحمل

1-Hatua ya kutokuwepo

2-kisha (hatua ya) mimba

ثم الدنيا
ثم البرزخ
ثم الآخرة

3- kisha (hatua ya) duniani .

4- kisha (hatua ya) kizuizini /kaburini

5- kisha (hatua ya) akhera

(شرح العقيدة الواسطية – ج٢ ص١٠٦)

Maelezo ya mfasiri :

Hizi ndizo hatua ambazo mwanadamu huzipitia:

Hatua ya kwanza ni hatua ya kutokuwepo kama alivyoitaja Allah -aliyetukuka -:

هَلْ أَتَى عَلَى الْإِنْسَانِ حِينٌ مِنَ الدَّهْرِ لَمْ يَكُنْ شَيْئًا مَذْكُورًا

Bila shaka ulimpitia Binadamu wakati mrefu katika zama,hakuwa kitu kinachotajwa.

الإنسان/١

Hatua ya pili ni tumboni kwa mama mwanadamu hukaa humo aghlabu miezi tisa .

Hatua ya tatu ni duniani ni haya maisha tunayoishi ambayo ni muda mchache mno na ni starehe yenye kudanganya ,kama alivyosema Allah :

وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ

Na hayakuwa maisha ya dunia ila ni starehe idanganyayo.

الحديد ٢٠

Hatua ya nne ni kaburini sehemu ambayo inazingatiwa ni kama kituo cha kusubiri siku ya mwisho na kaburini ni mwanzo wa siku ya mwisho kama alivyosema Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie –

” إِنَّ الْقَبْرَ أَوَّلُ مَنَازِلِ الْآخِرَةِ“

Hakika kaburi ni makazi ya kwanza ya akhera.

رواه الترمذي وابن ماجه

Hatua ya tano na ya mwisho ni siku ya mwisho ambayo ni siku ya malipo, na uwepo wa siku hii hauna shaka kama alivyosema Allah -aliyetukuka -:

وَأَنَّ ٱلسَّاعَةَ ءَاتِيَةٌ لَّا رَيْبَ فِيهَا وَأَنَّ ٱللَّهَ يَبْعَثُ مَن فِى ٱلْقُبُورِ

Na kwamba Kiama ni chenye kuja, hapana shaka ndani yake; na kwa hakika Allah atawafufua walio makaburini.

الحج ٧ .

Tunamuomba Allah azichukue roho zetu juu uislamu na sunnah.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 9, 1443H ≈ Jan 11, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *