FAIDA KUTOKA KATIKA QURAN.

Makala namba (13) .

قال تعالى :

Amesema Allah aliyetukuka -:

‏{ إِنَّ هَٰذَا الْقُرْآنَ يَهْدِي لِلَّتِي هِيَ أَقْوَمُ }

{ Hakika hii Quran inaongoza katika njia iliyonyooka kabisa }

اﻹسراء ٩

«فالقرآن أباح ‎تعدد الزوجات لمصلحة المرأة في عدم حرمانها من الزواج ،

Basi Quran imehalalisha kuoa wake wengi kwa ajili ya maslahi ya mwanamke katika kutomzuia na kuolewa,

ولمصلحة الرجل بعدم تعطل منافعه في حال قيام العذر بالمرأة الواحدة ،

Na kwa ajili ya maslahi ya mwanamume kwa kutokosekana manufaa yake katika hali (ambayo) mwanamke mmoja atakuwa na udhuru,

ولمصلحة الأمة ليكثر عددها فيمكنها مقاومة عدوها لتكون كلمة الله هي العليا

Na kwa ajili ya maslahi ya ummah ili idadi yake iongezeke na utaweza kupambana na adui wake ili dini ya Allah iwe juu.

‏فهو تشريع حكيم خبير لا يطعن فيه إلا من أعمى الله بصيرته بظلمات الكفر».

Basi huo ni uwekaji sheria wa mwenye hekima ,mjuzi, (na) hatii dosari ndani ya (sheria) hiyo isipokuwa yule ambaye Allah ameutia upofu ufahamu wake kwa giza la ukafiri.

📚أَضواء البيان للشيخ محمد الأمين الشنقيطي رحمه الله ٤٩٧/٣

Maelezo ya mfasiri :

Hizi ni miongoni mwa hekima za ruhusa ya kuoa wake wengi kama alivyotaja sheikh -Allah amrahamu -:

1- Inajulikana kuwa idadi ya wanawake ni wengi, na pia kuna wale wanaofiwa na waume zao, na walio achwa na bila katika hili la ruhusa ya kuoa wake zaidi ya mmoja kuna wapa nafasi wanawake kuolewa na lau ruhusa hii isingekuwepo basi wanawake wengi wangebakia bila kuolewa kwa hiyo ruhusa ya kuoa mke zaidi ya mmoja ina maslahi kwa wanawake!

2- Pia ruhusa hii ina maslahi kwa wanaume kwa sababu mwanamke anapatwa na dharura nyingi ambazo humzuia mume kustarehe na mkewe mfano mke anaweza akawa katika siku zake za mwezi, au akajifungua, akawa katika nifasi, kuchoka, kuumwa n.k

3- Pia kuoa wake zaidi ya mmoja kuna maslahi kwa uma wa kiislamu kwa sababu kufanya hivyo ni sababu ya kuongezeka idadi ya waislamu watakao weza kupambana na maadui zao ili dini ya Allah iwe juu.

Bila shaka mwenye kuiangalia sheria hii ya kiislamu hata akiwa si muislamu basi atabainikiwa kuwa hii ni sheria ya Allah mwenye hekima, mjuzi na hakuna mwenye kuitia dosari sheria hii ya kiislamu isipokuwa yule ambaye Allah amemtia upofu katika ufahamu wake kwa ukafiri aliokuwa nao.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo Mosi 26, 1443H ≈ May 27, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *