عن سفيان بن حسين الواسطي -رحمه الله- :
Kutoka kwa Sufian bin Husain Al-waasitwiy -Allah amrahamu (amesema) -:
«ذكرت رجلاً بسوء عند إياس بن معاوية المزني قاضي البصرة –
Nilimtaja mtu (mmoja) kwa ubaya mbele ya Iyas bin Mu’awiyah Al-Muzaniy kaadhi wa Al-Baswrah –
- وهو تابعي يَضرب المثل بذكائه-
-Naye (huyu Kadhi) ni tabi’iy anayepigiwa mfano kwa akili –
فنظر في وجهي وقال : أغزوت الروم ؟
Basi akanitezama usoni na akasema : Je wewe (umeshawahi) kupambana na Warumi ?
قلت : لا !
Nikajibu : Hapana!
قال : أفتسلم منك الروم والسند والهند والترك ، ولم يسلم منك أخوك المسلم ؟!
Akasema (Iyas) : Hivi (wewe upo vipi), wanasalimika na wewe Warumi na watu wa Sindi na Wahindi na Waturki , na hakusalimika na wewe ndugu yako muislamu ?!
قال سفيان : لم أعُد بعدها – يعني إلى عيب أحد من الناس أو غيبته -» .
akasema Sufian : Sikurudia tena baada ya hapo – anakusudia kuwa hakurudia tena kumuaibisha yeyote katika watu au kumsengenya .
انظر : “البداية والنهاية” لابن كثير (٣٣٦/٩) و”تهذيب الكمال” (٤٢١/٣) في ترجمة إياس بن معاوية المزني قاضي البصرة وفقيهها
Maelezo ya mfasiri :
Huyu Iyas bin Mu’awiyah Al-Muzaniy ambaye ni mwanafunzi wa Maswahaba alimwambia huyu Sufian bin Husain Al-waasitwiy kuwa : Makafiri wamesalimika na wewe kutokana na viungo vya mwili wako kwa maana haukuwahi kupambana nao katika jihadi, lakini muislamu mwenzako hajasalimika na wewe kutokana na ulimi wako ! , na aliitaja miji hii lakini anakusudia Makafiri wa maeneo hayo kipindi hicho.
Bila shaka hali imekuwa mbaya haswa katika zama zetu hizi ambazo usengenyi na umbea ni jambo la kawaida watu wengi na hata wale wanaojinasibisha na elimu ya kisheria wameshindwa kuzizuia ndimi zao ! , na hali Mtume -swala na salamu zimfikie -anasema :
الْمُسْلِمُ مَنْ سَلِمَ الْمُسْلِمُونَ مِنْ لِسَانِهِ وَيَدِهِ،
“ Muislamu mkamilifu ni yule ambaye wamesalimika Waislamu kutokana na (shari ya) ulimi wake na mikono yake ”.
Tanbih :
Mlango wa kuwajeruhi watu yaani kubainisha bidaa zao na upotevu wao haukufunguliwa wazi kwa kila mtu bali una vidhibiti vyake na kanuni zake ambazo huzijua wanawavyuoni na wanafunzi waliomakinika katika elimu, kwa hiyo asije mtu akaingia katika usengenyi kwa kujifichia katika mlango huu.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo Mosi 28, 1443H ≈ May 29, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•