Kadi namba (1) .
ياأيها الزوج :
Ewe mume :
يا من كرمه الله عز وجل بالقوامة على المرأة ،وجعل الطلاق بيده ،قال الله عز وجل :
Ewe (yule) ambaye Allah amemfadhilisha kwa kumpa usimamizi juu ya mwanamke na akaiweka talaka katika mkono wake ,amesema Allah -aliyeshinda na kutukuka -:
{الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاء بِمَا فَضَّلَ اللّهُ بَعْضَهُمْ عَلَى بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُواْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ }
Wanaume ni wasimamizi wa wanawake ,kwa sababu Allah amewafadhilisha baadhi yao juu ya wengine, na kwa sababu ya mali zao walizozitoa.
(النساء ٣٤)
تمهل ولا تتسرع فيه ، فإنما جعل الطلاق بيدك؛ لأنك الأعقل ،
Kuwa mpole na wala usifanye haraka katika (kuitoa) hiyo (talaka) ,na hakika si vinginevyo imewekwa talaka mkononi mwako kwa sababu wewe ni mwenye akili zaidi,
فتستطيع أن توازن بين المصالح والمفاسد؛
Unaweza kupima baina ya maslahi na mafasidi (mabaya)
أما المرأة فعاطفية تغلب جانب العاطفة على جانب العقل.
Ama mwanamke ni (kiumbe) mwenye shauku (ya kupita kiasi), upande (wake) wa shauku huwa na nguvu zaidi ya upande wa akili.
المصدر : الوصية الشرعية للحياة الزوجية ،للشيخ سعيد بن سالم الدرمكي
Maelezo ya mfasiri :
Maumbile ya mwanamke yanatofautiana na ya mwanamume na hapa utabainikiwa hekima ya Allah -aliyetukuka -kuiweka talaka kwa mwanamume , miongoni mwa maumbile aliyokuwa nayo mwanamke ni shauku ya hali ya juu katika kuyaendea mambo, huruma wa kupindukia, na uwezo wake wa kudhibiti mambo si kama mwanamume na haya ndiyo makusudio ya upungufu wa akili wa mwanamke ulioelezwa katika hadithi na wala haina maana kuwa mwanamke hana akili bali kuna wanawake wengi wanaowazidi wanamume kwa akili kama alivyosema ibn Taimiyyah -Allah amrahamu.
Wewe mwanamume ambaye Allah amekupa majukumu ya kumsimamia huyu mwanamke unawajibika kuwa na busara na utulivu katika kuamiliana na huyu mwanamke usizidiwe na shauku ya kufanya maamuzi bila ya kufikiri kwa kina kumbuka wewe ni mwanamume umefadhilishwa na kupewa nafasi !
Inaendelea.. Allah akitaka.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo pili 15, 1443H ≈ Jun 15, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•