MFULULIZO WA VIKADI VYA USIA WA KISHERIA WA MAISHA YA NDOA

Kadi namba (2) .

تذكر أيها الزوج أن الزواج نعمة من نعم الله عز وجل عليك

Kumbuka ewe mume kuwa ndoa ni neema katika neema za Allah -aliyeshinda na kutukuka -juu yako

فحافظ عليها ولا تفرط فيها،بسبب زلة يمكن تصحيحها،

Basi ichunge hiyo (neema) na wala usizembee katika hilo kwa sababu ya kosa linalowezekana kusahihishwa,

وهفوة يمكن تجاوزها ، وغفلة يمكن التغاضي عنها قال الله عز وجل :

(Au kwa sababu ya) kosa linalowezwa kusamehewa, na (kwasababu ya) kughafilika kunakowezwa kufumbiwa macho , amesema Allah -aliyeshinda na kutukuka -:

{ وَمِنْ ءَايَٰتِهِۦٓ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَٰجًا لِّتَسْكُنُوٓاْ إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَءَايَٰتٍۢ لِّقَوْمٍۢ يَتَفَكَّرُونَ }

Na miongoni mwa alama zake ni kuwa Amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mpate utulivu kwao,naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu.Bila shaka katika hayo zimo ishara kwa watu wanaofikiri.

الروم ٢١

المصدر : الوصية الشرعية للحياة الزوجية ،للشيخ سعيد بن سالم الدرمكي

Maelezo ya mfasiri :

Mume kupata utulivu kwa mkewe na mke kumuhitajia mumewe ni jambo la kimaumbile na baina yao kuna mapenzi makubwa na huruma kama alivyoeleza Allah , na bila shaka ametakasika Allah ambaye amewakusanya wawili hao -mwanamke na mwanamume -wawili ambao kabla ya hapo walikuwa hawana mahusiano yoyote isipokuwa udugu wa imani! lakini kitendo cha kufunga ndoa tu na kukutana kimwili wawili hao muda huo kunazalika faida hizi tatu :

1-Utulivu, 2- mapenzi, 3- huruma , kama alivyosema ibn Kathir -Allah amrahamu katika tafsiri ya aya hiyo katika suratul -Ruum -:

فإن الرجل يمسك المرأة إما لمحبته لها ، أو لرحمة بها ، بأن يكون لها منه ولد ،

Basi bila shaka mwanamume hubaki na mwanamke ima kwa kumpenda au kwa kumuonea huruma kwa (kutaraji kuwa) atapata mtoto

أو محتاجة إليه في الإنفاق ، أو للألفة بينهما ، وغير ذلك..

Au (huyo mwanamke) ni mwenye kumuhitajia katika kumlisha au kwa ajili ya kuzoeana kwao na (sababu nyingine) zisizokuwa hizo.

Tanbih :

Mume zingatia maisha haya ya ndoa hayawezi kudumu na wala utulivu huu hauwezi kupatikana isipokuwa pale wanandoa wawili na haswa mume atakapofumbia macho baadhi ya makosa na yale yanayopaswa kusahihishwa basi yasahihishwe kwa njia mzuri kama alivyosema sheikh -Allah amuhifadhi-.

Inaendelea.. Allah akitaka.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo pili 16, 1443H ≈ Jun 16, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *