Kadi namba (5) .
أيها الزوج :
Ewe mume :
قد وصاك -صلى الله عليه وسلم -بزوجتك خيرا ،فاقبل وصية نبيك ففيها سعادتك ،
Hakika amekuhusia (Mtume) -swala na salamu za Allah zimfikie -kwa mkeo (umfanyie) heri basi ukubali usia wa Mtume wako ndani yake kuna utulivu/ furaha yako ,
قال النبي -صلى الله عليه وسلم-:
” استوصوا بالنساء خيراً فإنهن عوانٍ عندكم“
Amesema Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -:
“ Usianeni baina yenu kuwafanyia wema hao (wanawake) hakika hao (wanawake) ni mateka kwenu ”
(آداب الزفاف ١٩٨) .
عوان :أي أسيرات ،فالمرأة تابعة للزوج،هو الذي يأمرها وهو الذي ينهاها ،وهو الذي ينفق عليها ،فترفق بها واصبر عليها.
Maana yake : (Wanawake) ni mateka ,mwanamke ni mwenye kumfuata mume yeye ndiye ambaye anayemuamrisha na yeye ndiye anayemkataza na yeye ndiye anayemlisha ,basi (ewe mume) muonee huruma na mvumilie
المصدر : الوصية الشرعية للحياة الزوجية ،للشيخ سعيد بن سالم الدرمكي
Maelezo ya mfasiri :
Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -amewausia wanaume waishi kwa wema na wake zao na huu ulikua ni miongoni mwa usia wake Mtume -swala na salamu za Allah -katika hija yake ya kuaga.
Tanbih :
Kauli yake Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -:
“Hakika hao (wanawake) ni mateka kwenu ” .
Maana yake:
Mume atilie umuhimu na pupa katika kumsimamia yale yanayohusu dini yake na dunia yake ni kwa sababu huyo mwanamke yupo chini ya mwanamume, ndiyo maana akafananishwa na mateka na wala haina maana anyanyaswe bali ni wajibu apewe haki zake za kisheria na ndiyo maana Allah amesema:
( وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ )
Na (wanawake) wanayo haki kwa sharia (kufanyiwa na waume zao) kama ile haki iliyo juu yao kuwafanyia waume zao .Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao .
البقرة : ۲۲۸ .
Na hivi ndivyo yalivyokuwa maisha yake Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- pamoja na wakeze -Allah awaridhie – yalikuwa ni maisha ya furaha na raha na kuamiliana nao kwa upole na wala haina maana kuwa asimuadabishe ila kama atamuadabisha basi afuate njia za kisheria, na yamethibiti maneno kutoka kwa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie – :
إنِّي أحرِّجُ حقَّ الضَّعيفينِ : اليتيمِ ، والمرأَةِ
Hakika mimi natahadharisha (kudhulumu) haki za wanyonge wawili : yatima na mwanamke
صحيح الجامع
الرقم ٢٤٤٧
Hii ni tahadhari kutoka kwa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -juu ya kuwadhulumu wanyonge hawa wawili : Yatima ni mtoto ambaye baba yake amefariki na hali hajabaleghe, na mwanamke pia ni mnyonge kwa maumbile yake na akili yake kwa hiyo mume anatakiwa achunge na atahadhari na kumdhulumu mkewe ambaye yeye amepewa jukumu la kumsimamia
Inaendelea.. Allah akitaka.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo pili 21, 1443H ≈ Jun 21, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•