MFULULIZO WA VIKADI VYA USIA WA KISHERIA WA MAISHA YA NDOA

MFULULIZO WA VIKADI VYA USIA WA KISHERIA WA MAISHA YA NDOA

Kadi namba (6) .

تذكر أيها الزوج :

Kumbuka ewe mume :

أنه لا يكاد يخلو بيت من مشكلة،ومن اختلاف في وجهات النظر،حتى بيت النبي -صلى الله عليه وسلم ،

Kwamba inakaribia (kutokuwepo) nyumba inayoepukana na matatizo ,na kutofautiana mitizamo hata nyumba ya Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie,

هل تعلم أن الله سبحانه وتعالى هدد زوجات النبي -صلى الله عليه وسلم-بالطلاق في القرآن، مع عظيم مكانتهم ،قال تعالى :

Je unajua kuwa Allah -utakasifu ni wake na ametukuka -aliwakhofisha wake za Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -na talaka katika Quran pamoja na ukubwa wa daraja lao, amesema (Allah) aliyetukuka -:

{ عَسَىٰ رَبُّهُۥٓ إِن طَلَّقَكُنَّ أَن يُبْدِلَهُۥٓ أَزْوَٰجًا خَيْرًا مِّنكُنَّ }

{Huenda Mola wake mlezi kama atakuacheni (Mtume wake) atambadilishia wake bora kuliko nyinyi }

(التحريم : ٥).

هل تعلم أن النبي -صلى الله عليه وسلم -هجر زوجاته شهرا كاملا ،فكان يبيت لوحده -صلوات الله وسلامه عليه .

Je unajua kuwa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -aliwahama wakeze mwezi mzima alikuwa akilala peke yake, -swala na salamu za Allah zimfikie-.

هل تعلم أن زوجات النبي -صلى الله عليه وسلم -كان يقع بينهن من الخصام ما يكون بين النساء الضرائر ؟
Je unajua kuwa wake za Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -yalikuwa yakitokea baina yao magomvi yale yanayotokea baina ya wake wenza.

المصدر : الوصية الشرعية للحياة الزوجية ،للشيخ سعيد بن سالم الدرمكي

Maelezo ya mfasiri:

Maisha ya ndoa hayaepukani na migongano hili tukio aliloliashiria shekhe amelitaja Allah-aliyetukuka- katika Surat Tahrim pindi mama Aisha na Hafswa -Allah awaridhie – kulifanya lile walilolifanya kwa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -Allah akawakhofisha na talaka, na pia Mtume -swala na salamu aliwahi kuwahama wakeze mwezi mmoja kamili kwa kosa walilolifanya la kumuomba Mtume -swala na salamu zimfikie -awazidishie matumizi na mavazi ya ziada kwa maana walitaka mapambo ya dunia ,basi Allah -aliyetukuka -akateremsha aya hizi za kuwakhiyarisha :

{ يَاأَيُّهَا النَّبِيُّ قُلْ لِأَزْوَاجِكَ إِنْ كُنْتُنَّ تُرِدْنَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا فَتَعَالَيْنَ أُمَتِّعْكُنَّ وَأُسَرِّحْكُنَّ سَرَاحًا جَمِيلًا }
Ewe Mtume! Waambie wake zako : “ Ikiwa mnapenda maisha ya dunia na mapambo yake, njooni nitakupeni kitoka nyumba, na kukuacheni muwachano mzuri. ”

وَإِنْ كُنْتُنَّ تُرِدْنَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَالدَّارَ الْآخِرَةَ فَإِنَّ اللَّهَ أَعَدَّ لِلْمُحْسِنَاتِ مِنْكُنَّ أَجْرًا عَظِيمًا}

Na kama mnamtaka Allah na Mtume wake na nyumba ya akhera, basi Allah amewaandalia wafanyao mema hayo, ambao ni nyinyi ,malipo makubwa

الأحزاب/٢٨-٢٩

Baada ya kuteremka aya hizi Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -aliwaita wakeze wote mmoja mmoja akawahiarisha na akaanza na mama Aisha na wake wa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -wote walimchagua Allah na Mtume wake na nyumba ya akhera kwa maana hawakuchagua maisha ya dunia.

Nukta nyingine :

Mikwaruzano baina ya wake za Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -ilikuwepo na hiyo mara nyingi haikosekani baina ya wake wenza kama ilivyothibiti katika hadithi:

“ Siku moja Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -alikuwa kwa mama Aisha -Allah amridhie -basi mmoja katika wakeze ima mama Zainabu au Swafiyyah -Allah awaridhie -akamtuma mtumishi na sahani ya chakula ampelekee Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie -basi mama Aisha akapiga mkono wa yule mtumishi na sahani ikavunjika basi Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie – akawa anakusanya vile vipande vya sahani iliyovunjika na kile chakula kilichomwagika kisha akawaambia wale waliopo hapo :

” كلوا غارَتْ أُمُّكم ..“

“ Kuleni mama yenu amepatwa na wivu” .

Kisha Mtume akamzuia yule mtumishi asiondoke ili mama Aisha -Allah amridhie -ailipe hii sahani aliyoivunja kisha akampatia yule mtumishi na ile iliyovunjika ikabakia kwa mama Aisha ”.

رواه البخاري والطحاوي في مشكل الآثار.

Faida kutoka kwenye tukio hili :

Uzuri wa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -katika kuamiliana na wakeze na kuchunga kwake hali yao ya wivu ,na pia hapa kunadhihiri uadilifu wake -swala na salamu za Allah zimfikie- na upole na busara pia.

Pia tunajifundisha kuwa wivu ni katika maumbile ya wanawake tena ni hali iliyowatokea wanawake waliokuwa bora kwa hiyo mume mwenye wake wengi anatakiwa alitambue hili na awe na busara katika kuamiliana nao.

Inaendelea.. Allah akitaka.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo pili 23, 1443H ≈ Jun 23, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *