Kadi namba (7) .
ياأيها الزوج :
Ewe mume :
ربك أمرك بالصبر على الزوجة ومعاشرتها بالتي هي أحسن
Mola wako amekuamrisha kuwa na subira juu ya mke na kuishi naye kwa namna ambayo ni mzuri,
ولو كنت كارها لها ،قال رب العزة سبحانه وتعالى :
Hata kama utakuwa ni mwenye kumchukia ,amesema Mola -mwenye nguvu na utakasifu ni wake na ametukuka -:
{ وَعَاشِرُوهُنَّ بِٱلْمَعْرُوفِ ۚ فَإِن كَرِهْتُمُوهُنَّ فَعَسَىٰٓ أَن تَكْرَهُواْ شَيْـًٔا وَيَجْعَلَ ٱللَّهُ فِيهِ خَيْرًا كَثِيرًا }
{Na kaeni nao kwa wema; na kama mkiwachukia basi (msiwaache) kwani huwenda mkakichukia kitu, na Allah akajaalia kheri nyingi ndani yake }
النساء ١٩
ومصداق ذلك من السنة قول نبينا محمد -صلى الله عليه وسلم- :
Na dalili ya ukweli wa hilo katika sunnah ni kauli ya Mtume wetu Muhammad -swala na salamu za Allah zimfikie -:
” لَا يَفْرَكْ مُؤْمِنٌ مُؤْمِنَةً، إنْ كَرِهَ منها خُلُقًا رَضِيَ منها آخَرَ،“
” Asimchukie muumini wa kiume muumini wa kike kama atachukia kutoka kwake tabia moja (basi) ataridhia kutoka kwake (tabia) nyingine.
رواه مسلم ١٤٦٩
المصدر : الوصية الشرعية للحياة الزوجية ،للشيخ سعيد بن سالم الدرمكي
Maelezo ya mfasiri:
Mume tambua kwamba ukichukia tabia fulani kwa mkeo basi kuna mazuri mengi kwake yanayokupendeza kama alivyoeleza mtume – swala na salamu za Allah zimfikie hapo juu na kabla ya hapo sheikh ametaja aya katika Quran yenye maana hiyo kuwa unaweza ukamchukia mkeo kwa tabia fulani aliyokuwa nayo lakini Allah akajaalia kheri nyingi kutoka kwake kama alivyotaja ibn Kathiri -Allah amrahamu -katika tafsiri ya aya hii kutoka kwa ibn Abbas -Allah amridhie -:
: هو أن يعطف عليها ، فيرزق منها ولدا . ويكون في ذلك الولد خير كثير
“ Huko ni (kule mume) kumuonea huruma huyo (mke) ,basi akaruzukiwa mtoto kwa (mwanamke) huyo na kukawa kwa huyo mtoto (kuna) kheri nyingi …” .
mume usiwe unaangalia kwa mkeo makosa aliyokuwa nayo tu bali angalia mema na mazuri aliyokuwa nayo hii itakusaidia katika kuishi nae na kumvumilia kutokana na baadhi ya tabia zake, na kule kumvumilia kunaweza kukawa ni sababu ya kupata kheri nyingi kama vile kupata watoto wema watakao kunufaisha duniani na akhera, au Allah ataibadilisha ile chuki uliyokuwa nayo ikawa ni mapenzi! .
Tanbih : Makusudio ya kumvumilia mke hapa kama kutakuwa hakuna madhara katika huko kumvumilia ama kukiwa na madhara basi ampe talaka, na vilevile haina maana mtu avumilie kuishi na mke muovu kama mzinifu n.k, bali makusudio ya kuvumilia ni baadhi ya tabia ambazo huwenda akawa nazo mke ambazo si mzuri kama vile kutotekeleza wajibu wake sawasawa n.k
Inaendelea.. Allah
akitaka.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo pili 27, 1443H ≈ Jun 27, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•