Makala namba (3) na ya mwisho.
للشيخ عبد الله بن صالح العبيد-حفظه الله-.
(Maneno ya) sheikh Abdullah bin Swaleh Al-ubaid -Allah amuhifadhi -.
مسائل مهمة في دراسة سيرة النبي -صلى الله عليه وسلم :
Masuala muhimu katika kuisoma sira ya Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie – :
“ Hakika kanuni na msingi kwa wanachuoni wakubwa waliobobea na waliohifadhi katika maimamu wa wema waliopita katika kuyapokea yale yaliyonukuliwa kwa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -(sira) yamegawanyika sehemu kuu tatu :
Kigawanyo cha tatu :
هو ما لم يشتهر بين أهل العلم وهذا كثير جدا تجده أحيانا عند أبي نعيم في دلائل النبوة وعند البيهقي ومن جاء بعدهم كابن عساكر ،
Hicho ni kile (kigawanyo) kisichokuwa mashuhuri baina ya wanawavyuoni, na (aina) hizi ziko nyingi mno utazikuta (aina hizi) muda mwingine kwa Abuu Nu’aim katika “Dalailu nnubuwa na kwa Al-baihaqiy na (pia) wale waliokuja baada ya hao
فهؤلاء أرادوا جمع ما وصل إليهم من السير ، ولهذا يكثر في هذا النوع المناكير التي التي استنكرها أهل العلم
Basi hawa (wanawavyuoni makusudio yao) walitaka kukusanya kile kilichowafikia katika sira (bila ya kupembua) ,na kwa ajili hii kunakithiri katika aina hii (riwaya) munkari ambazo wamezipinga wanawachuoni
فتجد مثلا البخاري أو أبا حاتم أو ابن المديني أو الإمام أحمد يستنكر مثل هذا الشئ
Utamkuta mfano Bukhariy au Abuu Hatim au ibn Al-madiniy au imamu Ahmad wakipinga mfano wa vitu hivi (kigawanyo hichi)
فهؤلاء يستنكرون مثل هذه المرويات التي تكثر في تلك الكتب .
Basi hawa (wanawavyuoni) huyapinga mfano wa haya yaliyopokewa ambayo hukithiri katika hivyo vitabu.
Maelezo ya mwandishi :
Kisha sheikh -Allah amuhifadhi – akaeleza kuwa kigawanyo hichi cha tatu ndicho ambacho wewe unaweza kupitisha maoni yako kwa kueleza kuwa hili limethibiti au halikuthibiti kwasababu yale yanayowafikia hao (waandishi) muda mwingine huwafikia kwa njia ya taabi’i taabi’in (wafuasi wa maswahaba) na hali hilo tukio halijawa mashuhuri baina ya taabi’i taabi’in katika zama hizo ima kwa sababu ya udhaifu wa tukio hilo au wameona kuwa hilo jambo halikusihi riwaya yake.
Na kigawanyo hichi cha tatu ambacho ndani yake kunakithiri yasiyokuwa sahihi kipo kwa wingi kwa wale waandishi wa sira wa karne ya nne, ya tano, ya sita mpaka karne ya nane, utakuta katika vitabu hivi vya sira kuna vitu vinatajwa ambavyo havina wapokeaji kabisa ni vitu tu walivisikia kwa watu na wakaviandika kwa hiyo kigawanyo hichi unaweza ukabainisha usahihi au udhaifu hakuna tatizo.
Ama yale matukio ya sira yaliyokuwa mashuhuri baina ya wanawavyuoni wameyasoma katika mikusanyiko mbalimbali, wameyasoma misikitini,katika vyuo kigawanyo hichi kiachwe kama kilivyo kama tulivyotaja katika makala namba mbili (2).
Tanbihi :
Misingi hii ya kuisoma sira ya Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -nimeitoa katika darsa yake sheikh -Allah amuhifadhi -alipokuwa anasherehesha kitabu cha mwanachuoni mkubwa Muhammad bin Abdil -Wahhab -Allah amrahamu -:
ستة مواضع من السيرة
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tatu 13, 1443H ≈ Jul 12, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•