MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUFU -AMANI IWE JUU YAKE –

Makala namba (27) .

قال الله تعالى عن يوسف-عليه السلام- :

Amesema Allah aliyetukuka kuhusu Yusuf -Amani iwe juu yake -:

{ يَا صَاحِبَيِ السِّجْنِ أَمَّا أَحَدُكُمَا فَيَسْقِي رَبَّهُ خَمْرًا ۖ وَأَمَّا الْآخَرُ فَيُصْلَبُ فَتَأْكُلُ الطَّيْرُ مِن رَّأْسِهِ ۚ قُضِيَ الْأَمْرُ الَّذِي فِيهِ تَسْتَفْتِيَانِ }

“Enyi wafungwa wenzangu wawili! Ama mmoja wenu atamnywesha bwana wake mvinyo. Na ama yule mwengine atasulubiwa ,na ndege watamla kichwa chake. Limekwishakatwa (limepita) hili jambo mlilokuwa mkiuliza”

سورة يوسف :٤١

Maelezo ya mfasiri :

Yusufu -amani iwe juu yake -baada ya kuwalingania katika tauhid na kumpwekesha Allah na kuacha kumshirikisha Allah akaanza kuwaagulia ndoto yao akawaambia bila ya kumuashiria mmoja mmoja bali alizungumza kwa ishara ili asihuzunike yule ambaye atauawa:

Ama mmoja wenu aliyekamua zabibu katika ndoto yake, yeye atatoka jela, na atakuwa akimnywesha ulevi Mfalme . Na ama huyu wa pili atatundikwa msalabani kabla ya kuuawa, na baada ya kuuawa ataachwa msalabani ndege wakimla kichwa chake.
Kisha Yusufu -amani iwe juu yake -akawaambi :Yamekwisha timia na kupita haya niliyoyaeleza kwa mujibu mlivyo nitaka nieleze tafsiri ya hizo ndoto!

Na hapa tunajifundisha kuwa haifai kwa mtu kujiingiza katika suala la kuagua ndoto kwa sababu hili jambo lina kanuni zake na misingi yake kwa ajili hii kuagua ndoto kumejaaliwa ni kutoa fatwa ,na Allah -aliyetukuka -amelizungumza hilo katika sura hii pale alipomzungumzia yule mfalme alisema hivi :

ۖ يَا أَيُّهَا الْمَلَأُ أَفْتُونِي فِي رُؤْيَايَ إِن كُنتُمْ لِلرُّؤْيَا تَعْبُرُونَ

{ Enyi wakubwa! Nambieni maana ya ndoto yangu ikiwa nyinyi mnaweza kufasiri ndoto }

سورة يوسف (٤٣)

Vilevile sehemu nyingine :

{ يُوسُفُ أَيُّهَا ٱلصِّدِّيقُ أَفْتِنَا}

“Yusufu ewe mkweli ! tueleze”

سورة يوسف ٤٦

Nasaha zangu :

Anatakiwa anayetaka kuagua ndoto atilie umuhimu kuzifahamu hadithi zilizokuja kutoka kwa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -katika kuagua ndoto na yale yaliyokuja kutoka kwa maswahaba na wema waliopita katika mlango huu ,na kama mtu hajui basi aache asije akaingia katika mlango wa kumsemea Allah uwongo na Mtume wake -swala na salamu za Allah zimfikie.

FAIDA :

ukitaka kujua aina za ndoto nenda katika channel yetu ya telegram andika : المقريزي kitakujia kisa cha kuvutia ambacho ndani yake tumetaja aina za ndoto.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tatu 14, 1443H ≈ Jul 13, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *