Kadi namba (8) .
يا أيها الزوج
Ewe mume :
تذكر أن الله نهاك عن ظلم المرأة بدون سبب إن هي أطاعت أمرك، يقول الله عزوجل :
Kumbuka kuwa Allah amekukataza kumdhulumu mwanamke bila ya sababu kama huyo (mwanamke) atatii amri zako ,anasema Allah -aliyeshinda na kutukuka:
{ ۖ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلَا تَبْغُواْ عَلَيْهِنَّ سَبِيلًا ۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا }
Na kama watakutiini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Allah ndiye aliye juu na Mkuu.
النساء ٣٤
المصدر : الوصية الشرعية للحياة الزوجية ،للشيخ سعيد بن سالم الدرمكي
Maelezo ya mfasiri :
Dhulma ni katika madhambi makubwa anasema Allah -aliyetukuka – :
يا عِبَادِي، إنِّي حَرَّمْتُ الظُّلْمَ علَى نَفْسِي، وَجَعَلْتُهُ بيْنَكُمْ مُحَرَّمًا، فلا تَظَالَمُوا،
“ Enyi wajawangu ! Hakika mimi nimeizuia nafsi yangu na dhulma ,na nimeifanya baina yenu kuwa ni haramu ,basi msidhulumiane … ”
رواه مسلم.
Na pia kuna katazo maalumu la kumdhulumu mwanamke nayo ni maneno kutoka kwa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie – pale aliposema :
إنِّي أحرِّجُ حقَّ الضَّعيفينِ : اليتيمِ ، والمرأَةِ
Hakika mimi natahadharisha (kudhulumu) haki za wanyonge wawili : yatima na mwanamke
صحيح الجامع
الرقم ٢٤٤٧
Hii ni tahadhari kutoka kwa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -juu ya kuwadhulumu wanyonge hawa wawili : Yatima ni mtoto ambaye baba yake amefariki na hali hajabaleghe, na mwanamke pia ni mnyonge kwa maumbile yake na akili yake kwa hiyo mume anatakiwa achunge na atahadhari na kumdhulumu mkewe ambaye yeye amepewa jukumu la kumsimamia
Inaendelea.. Allah akitaka.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tatu 20, 1443H ≈ Jul 19, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•