NASAHA ZENYE THAMANI KWA WANAFUNZI NA WALIMU PIA !

قال أيوب السختياني-رحمه الله تعالى :

Amesema Ayyub Al-Sakhtiyaniy -Allah aliyetukuka amrahamu -:

” إذا أردت أن تعرف خطأ معلمك فجالس غيره “

“Ukitaka kujua makosa ya mwalimu wako basi keti na (mwalimu mwingine) asiyekuwa yeye ”

سنن الدارمي ١ / ١٥٣

Maelezo ya mfasiri :

Mwanafunzi anatakiwa ajitahidi kusoma kwa masheikh mbalimbali kwa sababu elimu ni bahari isiyokuwa na ufukwe !, na kusoma kwa walimu mbalimbali kunachangia kupanuka ubongo wa mwanafunzi na kujua mambo zaidi ya yale aliyojifunza kwa mwalimu wake huyo na pengine mwalimu wake huyo akawa hayajui baadhi ya mambo , na pia wanatakiwa walimu wawahimize wanafunzi wao kujitahidi kwenda sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuongeza maarifa hata kwa kusafiri na hii ndiyo kawaida ya wema waliopita walikuwa wakisafiri umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta elimu .Pia walimu wasiwang’ang’anie wanafunzi na kuwazuia kutoka ili wakafaidike zaidi kwa sababu kufanya hivyo ni alama ya kutompendelea heri huyo mwanafunzi wake.

Mwalimu mwenye kumpendelea heri mwanafunzi wake ni yule anayependa mwanafunzi wake afikie daraja la juu zaidi yake, na hii ni alama ya ikhlaswi ama yule ambaye hapendi mwanafunzi wake awe juu zaidi yake huyu si mwalimu bora kwa sababu ana moyo mchafu na husuda .

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tatu 21, 1443H ≈ Jul 19, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
    •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *