MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUFU -AMANI IWE JUU YAKE –

Makala namba (30)

Amesema (Allah) aliyetukuka -:

وَقَالَ ٱلَّذِى نَجَا مِنْهُمَا وَٱدَّكَرَ بَعْدَ أُمَّةٍ أَنَا۠ أُنَبِّئُكُم بِتَأْوِيلِهِۦ فَأَرْسِلُونِ

Hapo akasema yule aliyeokoka katika wale wawili na akakumbuka baada ya muda (mrefu) : Mimi nitakwambieni tafsiri yake .Basi nitumeni.

يُوسُفُ أَيُّهَا ٱلصِّدِّيقُ أَفْتِنَا فِى سَبْعِ بَقَرَٰتٍۢ سِمَانٍۢ يَأْكُلُهُنَّ سَبْعٌ عِجَافٌ وَسَبْعِ سُنۢبُلَٰتٍ خُضْرٍۢ وَأُخَرَ يَابِسَٰتٍۢ لَّعَلِّىٓ أَرْجِعُ إِلَى ٱلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَعْلَمُونَ

“Yusufu Ewe mkweli! Tueleze hakika ya ng’ombe saba wanene kuliwa na ng’ombe saba dhaifu. Na mashuke saba mabichi na mengine makavu, ili nirejee kwa watu wapate kujua .

سورة يوسف : ٤٥-٤٦

Maelezo ya mfasiri :

Akasema yule mtu aliyeokoka miongoni mwa wale wawili aliokuwa nao nabii Yusuf gerezani, na akakumbuka usia wa Yusufu, baada ya kupita muda mrefu, neno “Ummah ” hapa lina maana ya muda kama vile katika kauli yake Allah -aliyetukuka -:

وَلَئِنْ أَخَّرْنَا عَنْهُمُ ٱلْعَذَابَ إِلَىٰٓ أُمَّةٍۢ مَّعْدُودَةٍۢ

Na tukiwacheleweshea (kuwaletea) adhabu mpaka muda uliokwisha hisabiwa..

سورة هود ٨

Basi yule mtu akawaambia :Mimi nitakwambieni tafsiri ya ndoto aliyoitaja mfalme. Nipelekeni kwa Yusufu mwenye elimu ya kuifasiri .

Baada ya hapo wakatoka na wakaenda kwa Yusufu na yote haya hayakutajwa hapa na huu ni ufasaha wa Quran wa kufupisha maneno kwa kuondoa baadhi ya sentesi (الإيجاز بالحذف).

Yule mtu ambaye alikuwa ni mtumishi wa mfalme wa kumletea mvinyo /ulevi alipofika kwa Yusufu akamwita :Yusufu! ewe uliyefikia ukomo katika ukweli ! .Tueleze nini maana ya ndoto ya ng’ombe saba wanene kuliwa na ng’ombe Saba waliokonda. Na ndoto ya mashuke saba mabichi na mengine yaliyokauka? Nataraji ukinijibu nirejee kwa watu nikiwa na hii tafsiri uliyoitoa, ili nao wapate kujua maana ya ndoto hii na uhakika wake ,na waijue hali yako na ujuzi wako na fadhila zako .

Na yule mtu alimuita Yusufu kwa sifa ya mkweli aliyefikia ukomo katika ukweli, kwa sababu aliishi naye gerezani na hajapatapo kusikia kwake uongo ,kama vile alivyomjua kabla ya hapo kuwa yeye ni katika wema pale walipomwambia pindi walipokuwa pamoja gerezani :

إِنَّا نَرَاكَ مِنَ الْمُحْسِنِينَ

kwa yakini sisi tunakuona wewe ni miongoni mwa watu wema ” (36).

Na Yusufu alipotafsiri ile ndoto ikawa ndiyo sababu ya kuokoka na kunyanyuka daraja lake.

Na hii inajulisha kuwa mtu aliyefanya wema na akawa mkweli basi Allah atamuokoa Kama vile Allah alivyowaokoa na kuwapa faraja wale watu watatu ambao waliacha kuhudhuria jihad ya vita vya Tabuki kwa sababu ya wema wao na ukweli wao.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tatu 22, 1443H ≈ Jul 21, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *