Makala namba (31)
قال تعالى عن يوسف -عليه السلام – :
Amesema (Allah) aliyetukuka – kuhusu Yusufu -amani iwe juu yake -.
قَالَ تَزْرَعُونَ سَبْعَ سِنِينَ دَأَبًا فَمَا حَصَدتُّمْ فَذَرُوهُ فِى سُنۢبُلِهِۦٓ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّا تَأْكُلُونَ
Akasema : “Mtalima miaka saba mfululizo kwa juhudi .Na mtakavyovivuna viacheni katika mashuke yake, isipokuwa kidogo mnatakachokila .
: ثُمَّ يَأْتِى مِنۢ بَعْدِ ذَٰلِكَ سَبْعٌ شِدَادٌ يَأْكُلْنَ مَا قَدَّمْتُمْ لَهُنَّ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّا تُحْصِنُونَ
“Kisha itakuja baadaye miaka saba ya shida (ukame,watu muda huo) watakula vile mlivyowawekea isipokuwa kidogo mtakachohifadhi (kwa ajili ya mbegu) ”
ثُمَّ يَأْتِي مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ عَامٌ فِيهِ يُغَاثُ النَّاسُ وَفِيهِ يَعْصِرُونَ
Kisha baada ya haya utakuja mwaka ambao katika mwaka huo watu watanyeshezewa mvua, na watakamua (matunda)
سورة يوسف ٤٧،٤٨،٤٩
Maelezo ya muandishi :
Basi Yusufu kwa wema wake na ukweli aliokuwa nao hakumkasirikia yule mtu na wala hakumwambia sikwambii, pamoja na kuwa Yusufu alidhulumiwa kwa kufungwa bila ya kosa na huyu mtu pia hakuufikisha ujumbe wake kwa mfalme, lakini yeye akawatafsiria ile ndoto lakini pia aliwapa nasaha na tahadhari , na hapa tunajifundisha kuwa mtu mwema hasubiri malipo kutoka kwa watu wala shukurani bali yeye hutaraji malipo kutoka kwa Allah, Yusufu akasema :
Tafsiri ya ndoto hii ni kuwa mnatakiwa mlime katika ardhi ya ngano, na shairi kwa muda wa miaka saba mfululizo kwa ukulima wa juhudi.
Tanbih :
Na hapa katika aya imekuja habari lakini maana yake ni amri
“Mtavuna miaka saba kwa juhudi”, maana yake anawaamrisha :Walime kwa juhudi kama ilivyokuwa kawaida yao.
Kisha akawaambia:
Mtachovuna kihifadhini, mkiache katika mashuke yake, na wala musikoboe ili zisiharibike kwa hali ya hewa na wadudu isipokuwa kidogo mtachokila katika miaka hiyo ya njaa, kwa uangalizi mzuri.
Kisha baada ya miaka hii ya neema itakuja miaka saba ya ukame. Mtakula kile mlichokiweka akiba, isipokuwa kidogo mtachokihifadhi kwa ajili ya mbegu.
Faida :
Unaruhusiwa kuisifu na kuielezea miaka kuwa ina ukame kwa njia ya kutoa habari, kama vile kauli yake nabii Luti -amani iwe juu yake -baada ya kuwaona wale Malaika waliokuja katika sura ya vijana wazuri akadhani kuwa watu wake hawatowaacha :
وَقَالَ هَٰذَا يَوْمٌ عَصِيبٌ
“Hii ni siku ngumu (yenye shari) ”
هود ٧٧
Kwa hiyo kuuelezea wakati fulani kuwa una njaa au ukame n.k ni jambo linaloruhusiwa lakini isiwe kwa njia ya kuchukia na kulalamika.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tatu 22, 1443H ≈ Jun 21, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•