عن خالد بن رباح وهو أخو بلال بن رباح -رضي الله عنهما :
Kutoka kwa Khalid ibn Rabah naye ni ndugu wa Bilal ibn Rabah -Allah awaridhie -:
الناس ثلاثة أثلاث:
فسالم وغانم وشاجب.
Watu wamegawanyika vigawanyo vitatu :
Mwenyekusalimika, na mwenyekuchuma, na mwenyekubwabwaja.
قال: السالم : الساكت
والغانم: الذي يأمر بالخير وينهى عن المنكر، فذلك في زيادة من الله.
والشاجب:
الناطق بالخَنا والمعين على الظلم.
Akasema : Mwenyekusalimika (ni) mwenye kunyamaza.
Na mwenyekuchuma :(Ni) yule ambaye anaamrisha mema na anakataza maovu, basi huyo yupo katika ziada inayotoka kwa Allah.
Na mwenyekubwabwaja : Ni mwenye kuzungumza machafu na mwenye kusaidia dhulma.
صحيح/ابن أبي شيبة ٣٦٧٢٩
Maelezo ya mfasiri :
Hivi ndivyo vigawanyo vya watu :
1- Aliyenyamaza : Ni yule ambaye hakuchuma chochote katika thawabu na wala hakuyazungumza yale yatakayomfanya apate madhambi kwa maana huyu ameuzuia ulimi wake .
2- Na mwenye kuchuma ni yule aliyechuma ujira na thawabu kwa kuamrisha kwake mema na kukataza kwake mabaya, huyu ni yule mwenye kuutumia ulimi wake katika kheri.
3- Mwenye kubwabwaja ni yule mwenye kuzungumza machafu na huyu ni mwenye kupata madhambi na kuangamia, huyu ni yule aliyeshindwa kuuzuia ulimi wake matokeo yake akaangamia.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nne 5, 1443H ≈ Aug 3, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•