➡️ Makala namba ( 21)
🌱 ودليل الإستعاذة قوله تعالى :
Na dalili ya kutaka kukingwa ni kauli yake (Allah) aliyetukuka
↩️{قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الفَلَقِ }
Sema :najikinga kwa mola wa mapambazuko.
↩️وقوله تعالى:
🌱قُلْ أَعُوْذُ بِرَبِّ النَّاسِ
Na kauli yake (Allah) aliyetukuka :
Sema: najikinga kwa mola wa wanaadamu.
✍️Maelezo yanayotokana na sherhe za wanachuoni mbalimbali:
ೄྀ࿐ ೄ࿐ೄྀ࿐ ೄ࿐ೄྀ࿐
Kujikinga: ni kukimbilia kwa yule ambaye atakuzuia na yenye hatari unayoyaogopa ili yasikupate.
Na kujikinga ni katika aina za ibada,kwa hiyo haifai kujikinga kwa asiyekuwa Allah
na kujikinga kuna aina kadhaa na kila aina ina hukumu yake :
1️⃣ Kujikinga kwa Allah aliyetukuka nako kumekusanya ukamilifu wa wewe kumhitajia Allah na kukimbilia kwake na kuitakidi kwamba Allah ndiye anayetosha,na ndiye anayeweza kukuhami kutokana na kila kitu chenye shari kilichoko sasa hivi na kijacho,kikubwa na kidogo katika binaadamu na asiyekuwa bidaamu.
2️⃣ Kujikinga kwa sifa miongoni mwa sifa zake Allah, kama vile maneno yake na ukubwa wake na utukufu wake, na dalili ya hilo ni kauli yake Mtume- swala na salam za Allah ziwe juu yake-pale alipotaja dua ya kujikinga pindi mtu anapotaka kushuka sehemu fulani akasema :
أَعـوذُ بِكَلِـماتِ اللّهِ التّـامّاتِ مِنْ شَـرِّ ما خَلَـق
“ Najikinga kwa maneno ya Allah yaliyotimia kutokana na shari ya alivyoviumba ”
رواه مسلم
3️⃣ Kujikinga kwa maiti au aliye hai lakini yupo mbali na wewe na hawezi kukukinga bila shaka huu ni ushirikina mkubwa, kwa sababu kitendo cha kumuomba maiti akukinge bila shaka unaitikadi kuwa huyo maiti anakusikia na atakusaidia kwa maana anajua kile unachokihitaji kutoka kwake , na pia yule mwenye kumuomba hifadhi mtu ambaye yupo mbali na yeye bila shaka mtu huyu anaitikadi kuwa mtu huyo anamsikia na anajua ghaibu ! , na bila shaka huu ni ukafiri , na kuhusu hili amesema Allah aliyetukuka
{وَأَنَّهُۥ كَانَ رِجَالٌ مِّنَ ٱلْإِنسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٍۢ مِّنَ ٱلْجِنِّ فَزَادُوهُمْ رَهَقًا}
{Na hakika walikuwako wanaume miongoni mwa wanaadamu wakijikinga kwa wanaume miongoni mwa majini kwa hivyo wakawazidishia uwoga.}
سورة الجن ٦
Na waarabu walikuwa pindi wanaposhuka sehemu husema mmoja wao:
: ” أعوذ بسيد هذا الوادي من سفهاء قومه “
“Najikinga kwa bwana wa bonde hili kutokana na wapumbavu (ambao) ni watu wake “.
Kwa maana alikuwa mmoja wao anapofika jangwani hujikinga kutokana na shari za majini wa eneo hilo kwa mkubwa wao ili awazuie wale majini wadogo wasimdhuru .
Na Mtume -swala na salam za Allah ziwe juu yake-akalibatilisha hilo na akabainisha badala yake yasemwe maneno haya kujikinga kwa Allah, akasema :
مَن نزل مَنْزِلًا فقال : أعوذُ بِكلماتِ اللهِ التَّامَّاتِ من شرِّ ما خَلقَ ، لَم يَضرَّهُ شَيءٌ حتى يَرْتَحِلَ مَن مَنْزِلِه
“Mwenye kushuka sehemu yoyote akasema:
“ Najikinga kwa maneno ya Allah yaliyotimia kutokana na shari ya alivyoviumba” , basi hakitomdhuru chochote mpaka aondoke sehemu hiyo”.
4️⃣ Kujikinga kwa yule ambaye anaweza kukukinga katika viumbe katika binaadamu au sehemu au vinginevyo ambavyo vina uwezo wa kukukinga , na hili linafaa na dalili yake ni kauli yake Mtume -swala na salam za Allah ziwe juu yake-pale alipotaja fitna akasema :
ومَن وجَدَ مَلْجَأً أوْ مَعاذًا فَلْيَعُذْ بهِ.
“Na atakayepata sehemu ya kukimbilia basi akimbilie au sehemu ya kujikinga basi ajikinge”
رواه البخاري .
Na hili la mwisho baadhi ya wanavyuoni wanaona kuwa haifai mtu kujikinga kwa kiumbe chochote kwa sababu kujikinga ni katika ibada za moyo haifai kupelekwa kwa asiyekuwa Allah, ama hawa walioruhusu wao wameangalia udhahiri kwa maana likiwa ni jambo la kidhahiri ambalo kiumbe kinauwezo wa kumkinga mwanadamu basi hakuna katazo kikiwa hicho kiumbe kiko hai,na kinasikia ,kipo karibu na huyo mwenye kuomba kukingwa ,na kinauwezo .
Imepitiwa na : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: 16 Mfungo nne 1443H ≈ 14 Aug 2022M.