Kadi namba (12) .
تذكري أختي الزوجة:
Kumbuka dada yangu (ewe) mke :
أن محاولتك الصلح مع زوجك قبل النوم من علامات نساء أهل الجنة،
Kwamba kujaribu kwako kufanya sulhu na mumeo kabla ya kulala ni katika alama za wanawake wa watu wa peponi,
قال صلى الله عليه وسلم :
Amesema -swala na salamu za Allah zimfikie-:
” نِساؤكم مِن أهلِ الجنَّةِ الوَدُودُ الوَلودُ
Wake zenu (ambao ni) katika watu wa peponi ni (wale) wenye kuwapenda sana waume zao, wenye kuzaa sana
العؤود على زوجها ،
mwenye kurejea mno kwa mumewe ,
الَّتي إذا غضب جاءت حتى تضع يدها في يد زوجها، وتقول :
(mwanamke) ambaye anapokasirika (mumewe) huja (kwa mumewe) mpaka akaweka mkono wake katika mkono wa mumewe na husema:
لا أذوقُ غَمْضًا حتَّى تَرْضى“
“ Sitoonja usingizi mpaka uridhie ”
السلسلة الصحيحة ٢٨٧
المصدر : الوصية الشرعية للحياة الزوجية ،للشيخ سعيد بن سالم الدرمكي
Maelezo ya mfasiri:
Miongoni mwa alama za wanawake wa peponi ni hizi :
1- Wenye kuwapenda mno waume zao na haya mapenzi hudhihiri katika matendo yao .
2- Wenye kuzaa sana, na pia wapo tayari kuzaa sana na wala hawana sifa ya wanawake walioathirika na maneno ya makafiri wanaohimiza watu wasizae watoto wengi kwa kuchelea ugumu wa maisha ! .
3- kujitahidi kumridhisha mumewe pindi anapokasirika au hata anapokasirika yeye mke, na hilo hulifanya kabla ya kulala hakubali kulala mpaka ahakikishe mumewe karidhia na humwambie mumewe : Mimi nipo katika miliki yako sitopata usingizi mpaka uridhie .
Inaendelea.. Allah akitaka.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nne 18, 1443H ≈ Aug 16, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•