KWANINI ALLAH AMEWAFANANISHA WANAFIKI NA MAGOGO YALIYOEGEMEZWA ?

✍🏻قال العلامة ابن القيم -رحمه الله-:

Amesema mwanachuoni mkubwa ibn Al-qayyim -Allah amrehemu-:

«شبه الله -تعالى- المنافقين بالخشب المسنّدة، لأنهم أجسامٌ خاليةٌ عن الإيمان والخير.

Allah-aliyetukuka- amewafananisha wanafiki na magogo yaliyoegemezwa kwa sababu wao ni viwiliwili vilivyoepukana na imani na kheri.

⏪وفي كونها مسنّدة نكتة أخرى: وهي أن الخشب إذا انتفع به، جعل في سقفٍ أو جدارٍ أو غيرهما من مظان الانتفاع،

Na kuwa kwake (magogo) yaliyoegemezwa (kuna) faida:

Nayo ni kuwa : Magogo yatapokuwa yana manufaa huwekwa katika paa au ukutani au (sehemu) nyengine zisizokuwa hizo katika sehemu (zinazoleta) manufaa,

وما دام متروكاً فارغاً غير منتفعٍ به جعل مسندا بعضه إلى بعض، فشبه المنافقين بالخشب في الحالة التي لا ينتفع فيها بها».

Na maadamu yameachwa bila ya kazi (na) hayanufaishi, yakaegemezwa mengine juu ya mengine,basi (Allah) akawafananisha wanafiki na magogo katika hali ambayo hakuna manufaa yoyote katika (magogo) hayo .

📘[أعلام الموقعين (٣٧٩/١)].


Maelezo ya mpitiaji :

Hii ndiyo sababu ya Allah -aliyetukuka- kuwafananisha wanafiki na magogo yaliyoegemezwa ,yasiyokuwa na kazi yoyote pale aliposema :

كَأَنَّهُمْ خُشُبٌ مُّسَنَّدَةٌ ۖ

{ Lakini wao ni kama magogo yaliyoegemezwa }

سورة المنافقون ٤

Kama alivyosema ibn l-Qayyim- Allah amrahamu- kuwa wamefananishwa na magogo kwa sababu wanafiki wameepukana na imani na kheri mfano wao ni kama magogo yaliyotupwa na kuachwa yakaangukiana na yakawa hayana manufaa yoyote

Na makusudio ya wanafiki hapa na wale wanaodhihirisha uislamu na kuficha ukafiri katika nyoyo zao na miongoni mwa alama zao ni kuuchukia uislamu, na kufurahi pindi waislamu wanapopata shida na misukosuko , na hawa ndiyo wale ambao Allah ameeleza kuwa watakuwa katika tabaka ya chini kabisa ya moto wa Jahannah , pale aliposema :

{ إِنَّ ٱلْمُنَٰفِقِينَ فِى ٱلدَّرْكِ ٱلْأَسْفَلِ مِنَ ٱلنَّارِ وَلَن تَجِدَ لَهُمْ نَصِيرًا }

{ Bila shaka wanafiki watakuwa katika tabaka ya chini kabisa katika moto. Hutamkuta kwa ajili yao mwenye kuwanusuru (yeyote) }

سورة النساء ١٤٥

Mpitiaji : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nne 20, 1443H ≈ Aug 18, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *