➡️ Makala namba ( 22)
↩️ودليل الاستغاثة قوله تعالى :
Na dalili (ya kua kutaka kuokolewa ni katika ibada)ni kauli yake Allah aliyetukuka:
🌱{ إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَاسْتَجَابَ لَكُم }
Kumbukeni mlipokuwa mkiomba msaada kwa Mola wenu, akakujibuni.
surat Al amfaal aya ya (9)
Maelezo yanayotokana na sherhe za wanachuoni mbalimbali:
ೄྀ࿐ ೄ࿐ೄྀ࿐ ೄ࿐ೄྀ࿐
Istighaatha: Maana yake ni:
Kutaka kuokolewa kutokana na shida kubwa inayoangamiza nayo inavigawanyo vinne:
1️⃣ Kuomba kuokolewa na Allah- aliyetukuka na kushinda- na hii ni katika matendo bora zaidi na yaliyokamilika zaidi nao ni mwenendo wa Mitume na wafuasi wao .
na dalili ya hilo ni kauli yake Allah katika hii aya aliyoitaja sheikh , na aya hii ilishuka katika vita vya Badri pale Mtume swala na salam za Allah ziwe juu yake alipowaangalia washirikina ambao walikuwa wamefikia idadi ya watu alfu moja,na hali ya kuwa idadi ya Maswahaba ilikuwa ni watu mia tatu na kumi, basi Mtume swala na salam za Allah ziwe juu yake akawa anaomba dua akisema :
«اللهمَّ أَنْجِزْ لي ما وعدْتَني، اللهم آتِ ما وعدْتَني، اللهمَّ إنْ تَهْلِك هذه العِصابةُ من أهْل الإسلام لا تُعْبَد في الأرض
“ewe Allah nitimizie yale uliyoniahidi,ewe Allah nipe yale uliyoniahidi, ewe Allah ikiwa kitaangamia hiki kikundi katika waislam hutoabudiwa katika ardhi”.
ameipokea Muslim hadith namba (1763)
2️⃣ Kutaka msaada wa kuokolewa kwa maiti, au walio hai lakini hawapo na hawana uwezo wa kuokoa, basi tendo hili hukumu yake ni ushirikina, kwa sababu mwenye kufanya hivyo bila shaka atakuwa anaamini na kuitikadi kuwa hao anaowataka msaada wanauwezo wa kuendesha mambo kwa siri katika ulimwengu na ndio maana anawaomba msaada huo hali wao ni maiti au hawapo eneo hilo .
3️⃣ Kuomba kuokolewa kwa aliyehai katika yale anayoyajua na kuweza kuokoa, hili linafaa kama alivyosema Allah katika kisa cha nabii Mussa amani juu yake :
{فَٱسْتَغَٰثَهُ ٱلَّذِى مِن شِيعَتِهِۦ عَلَى ٱلَّذِى مِنْ عَدُوِّهِۦ فَوَكَزَهُۥ مُوسَىٰ فَقَضَىٰ عَلَيْهِ ۖ }
{Basi yule jamaa yake alimuomba msaada juu ya yule adui yake.Musa akampiga ngumi, akammaliza (akafa hapohapo) hali ya kuwa hajakusudia kumuua}
surat alqaswasw aya ya (15)
4️⃣ Kuomba kuokolewa kwa aliye hai ambaye hawezi bila kuitakidi moyoni kuwa ana nguvu za kisirisiri, mfano mtu anayezama majini akataka
kuokolewa na mtu mwenye maradhi ya kupooza, basi huu ni upuuzi na kejeli, jambo hili halifai kwa sababu huku ni kumdhihaki huyu mtu ,na sababu nyengine ya kuharamishwa hili ni kwa sababu mtu anaweza akahadaika na akadhania kwamba huyu mtu mwenye maradhi ya kupooza ana uwezo wa kuokoa.
TANBIHI:
Yafuatayo ni masharti ya kuruhusiwa kuomba msaada wa kuokolewa na kiumbe :
1-Anayeombwa msaada wa kuokoa awe hai ama akiwa maiti haifai kuombwa kwa sababu huo ni ushirikina.
2- Anayeombwa msaada wa kuokoa awepo mfano haifai kutaka msaada wa kuokolewa kwa Jibril pamoja na kuwa Jibril yupo hai na anauwezo lakini hayupo
3- Anayeombwa msaada wa kuokoa awe ana uwezo wa kuokoa ,ama kama hana uwezo wa kuokoa katika hiyo shida na muombaji akamtaka msaada wa kumuokoa hali moyo wake umeegemea kwake kuwa ana uwezo wa kumuokoa basi huo ni ushirikina .
4-Anayeombwa msaada wa kuokoa asikie, kwa maana lau huyu anayeombwa akiwa hai na anauwezo na yupo mahali husika lakini akawa hasikii mfano akiwa kiziwi itakuwa haifai .
Imepitiwa na : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nne 25, 1443H ≈ Aug 23, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•