(عن القاضي أبي يوسف، قال:
Kutoka kwa kadhi Abuu Yusuph ,amesema :
بينما أنا أمشي مع أبي حنيفة، إذ سمعت رجلاً يقول لآخر: هذا أبو حنيفة لا ينام الليل.
Muda ambao nilikuwa nikitembea pamoja na Abuu Hanifa, ghafla nikamsikia mtu akimwambia (mtu) mwingine (hivi) :
“ Huyu ndiye Abuu Hanifah (ambaye) halali usiku (kwa ibada)”
فقال أبو حنيفة:
Basi Abuu Hanifa (aliposikia) akasema:
والله لا يُتَحَدَثُ عني بما لم أفعل، فكان يحيي الليل صلاةً وتضرعًا، ودعاءَ)
“ Naapa kwa Allah ! kusizungumzwe (lolote) kuhusu mimi lile nisilolifanya” , na alikuwa (Abuu Hanifah) akihuisha usiku kwa kuswali ,na kunyenyekea na kuomba dua
سير أعلام النبلاء (٦/٨٩٩)
Maelezo ya mfasiri :
Hii ni miongoni mwa tofauti baina yetu na wema waliopita ,wenzetu walikuwa hawapendi kumsikia mtu akitaja mema yao na ibada zao walizokuwa wakizifanya kwa sababu walikuwa na hofu ya kujiingiza katika riyaa yaani kufanya matendo ili watu wawaone ,lakini sisi katika zama hizi tunapenda kusikia watu wakiyataja mema yetu na ibada zetu ,na tena tunapenda kuwasikia watu wakiyataja yale ambayo hatujayafanya katika mema na kheri mbalimbali !.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tano 5, 1443H ≈ Sept 1, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•