قال الشيخ ابن عثيمين رحمه الله:
Amesema sheikh ibn Uthaimin -Allah amrahamu-:
🔺 لا حرج على الإنسان أن يسأل الله تعالى إصلاح معاشه لقول النبيﷺ
Hakuna ubaya kwa mtu kumuomba Allah -aliyetukuka- kumtengenezea maisha yake kwa kauli yake Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie-:
(وأصلح لي دنياي التي فيها معاشي).
{Na nitengenezee dunia yangu ambayo ndani yake kuna maisha yangu}.
وكل إنسان يريد أن تصلح دنياه؛ لأنها لو فسدت لكان ذلك سبباً في فساد دينه،
Kila mwanadamu anataka itengemae dunia yake kwa sababu hiyo (dunia) ikiharibika itakuwa ni sababu ya kuharibika dini yake,
ولأن الإنسان إذا اشتغل بتحصيل معاشه فربما يصده عن أشياء كثيرة من الدين.
Na ni kwa sababu mwanadamu atakapojishughulisha na (mambo ya) kuyapata maisha yake (ya dunia) huwenda yakamzuia mengi katika dini .
📖 شرح بلوغ المرام (١٥/ ٥٤٨).
Maelezo ya mfasiri:
Haya maneno ni sehemu ya dua ndefu yenye faida kubwa ambayo Mtume -swala na salamu za Allah -alikuwa akiisoma na kipande hiki kina maana hakuna ubaya mtu kumuomba Allah amtengenezee dunia yake na pia hakuna ubaya wa kuitilia umuhimu dunia yake lakini kwa sharti asiitangulize juu dini kwa maana dini iwe ndiyo ya kwanza .
Kama alivyoeleza sheikh -Allah amrahamu- kuwa kila mtu anapenda dunia yake itengemae kwa sababu kama dunia itamuharibikia mtu akawa siku zote anahangaika na kuitafuta na kuikusanya basi bila shaka hiyo huwenda ikawa ni sababu ya kuharibikiwa katika dini yake !.
Dua yenyewe kwa ukamilifu wake ni hii :
اللَّهُمَّ أَصْلِحْ لي دِينِي الذي هو عِصْمَةُ أَمْرِي، وَأَصْلِحْ لي دُنْيَايَ الَّتي فِيهَا معاشِي، وَأَصْلِحْ لي آخِرَتي الَّتي فِيهَا معادِي، وَاجْعَلِ الحَيَاةَ زِيَادَةً لي في كُلِّ خَيْرٍ، وَاجْعَلِ المَوْتَ رَاحَةً لي مِن كُلِّ شَرٍّ
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tano 7, 1444H ≈ Sep 3, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•