أحاديث المهدي العلماء قسموها إلى أربعة أقسام :
Hadithi za Mahdi wanachuoni wamezigawanya vigawanyo vinne :
١- صحيحة.
٢- حسنة.
٣- ضعيفة.
٤- موضوعة.
1- Sahihi .
2-Hasan .
3-Dhaifu .
4- za uwongo .
✅ والراجح من أقوال أهل العلم: أنه سوف يأتي إذا دعت ضرورة الأرض إلى مجيئه.
Na kauli iliyokuwa na nguvu katika kauli za wanachuoni :Kuwa (Mahd) atakuja pindi itapokuwa kuna dharura ya kuja kwake (hapa) ardhini.
كأن تُمْلأ ظلماً وجوراً؛
Kama vile (mfano) ardhi (ikiwa) imejazwa dhulma
ولكنه هذا المهدي الذي من عقيدة أهل السنة والجماعة ليس هو مهدي الرافضة الذي ينتظرونه.
Lakini huyu Mahd ambaye (kumuamini) ni katika itikadi ya Ahlu sunnah wal-jamah si yule Mahd wa Mashia ambaye wanamsubiri.
فإن مهدي الرافضة الذي ينتظرونه ليس إلا خيالاً في أذهانهم، ولا حقيقة له. فهم يعتقدون أن المهدي هذا في السرداب الذي في العراق،
Na bila shaka Mahd wa Mashia ambaye wanamsubiria hayupo isipokuwa ni mazingaombwe tu (yaliyopo) katika akili zao na wala si kweli .Na wao (Mashia) wanaitikadi kuwa huyu Mahd yupo katika pango ambalo lipo Iraq,
وينتظرون خروجه كل يوم، وهذا لا أصل له، ولا حقيقة له، لا من الناحية التاريخية، ولا من الناحية العقلية.
Na husibiri kutoka kwake kila siku , na hili (wanaloliamini) halina dalili na wala halina ukweli si katika upande wa kihistoria wala upande wa kiakili
🎙 المصدر: لقاء الباب المفتوح لابن عثيمين [١].
Maelezo ya mfasiri:
Huyu ndiye Mahd ambaye atatokea mwishoni mwishoni mwa dunia kabla ya kushuka Isa bin Mariam -Amani iwe juu yake- na kutokea kwake ni miongoni mwa alama za kiama kubwa kubwa , ambaye atawaongoza waislamu na kuujaza ulimwengu uadilifu ,na kama alivyoeleza sheikh -Allah amrahamu- kuwa Ahlu sunnah tunaamini kuwa huyu Mahd atatokea na atakuwa ni katika kizazi cha Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- kama alivyosema Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie-:
” لا تقومُ السَّاعةُ حتى يَملِكُ رجُلٌ من أهلِ بَيْتي،
Hakitosimama Kiama mpaka amiliki (atawale) mtu katika watu wa nyumbani kwangu ,
أَجْلى أَقْنى، يَملَأُ الأرضَ عَدلًا، كما مُلِئَتْ قبْلَه ظُلمًا، يكونُ سَبعَ سنينَ “.
“ (sifa zake ni hizi) hana nywele mbele ya kichwa chake , paji lake la uso ni pana, mwenye pua ndefu iliyochongoka, ataujaza ulimwengu uadilifu kama (ulivyokuwa ulimwengu )kabla ya yake ulijazwa dhulma , na (utawala wake) utakuwa kwa muda wa miaka saba ”
أخرجه أحمد (١١١٣٠) واللفظ له، وأبو يعلى (١١٢٨).
Tanbih :
Shekhe -Allah amrahamu- ametoa tahadhari kuwa Mahd tunayemuamini sisi Ahlu ssunaah si yule wanayemuamini Mashia ambaye ni Mahd wa kubuni na wa uwongo na hayupo, na katika vituko vyao hao Mashia huwa wanamsubiria huyo Mahd huko Iraq katika pango wanadai kuwa atatoka hako na hili hulifanya kila siku !
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tano 8, 1443H ≈ Sep 5, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•