◾️ قال ابن رجب الحنبلي -رحمه الله-:
Amesema ibn Rajab Al-Hanbaliy -Allah amrahamu-:
“فمن فعل محرَّماً مرَّةً، ثم عزم على فعله متى قَدَرَ عليه، فهو مُصِرٌّ على المعصية،
Basi mwenye kufanya haramu mara moja kisha akaazimia kufanya (tena) muda atakaoweza,basi (mtu) huyo ni mwenye kuendelea (kufanya) maasi,
ومعاقَبٌ على هذه النية، وإن لم يَعُدْ إلى عمله إلاّ بعد سنين عديدة.
Na ni mwenye kuadhibiwa juu ya hii nia hata kama hajarudia kufanya hayo (maasi) ila baada ya miaka mingi.
وبذلك فسّر ابنُ المبارك وغيرُه الإصرار على المعصية”.
Na hivyo ndivyo alivyofasiri ibn l-Mubarak na wengineo maana ya kuendelea na maasi .
📚جامع العلوم والحكم، لابن رجب (٣٢٧/٢)
Maelezo ya mfasiri:
Mwenye kufanya uovu kisha akakusudia kurudia tena uovu huo basi bila shaka mtu huyo kama atakuwa ametubu basi toba yake haikubaliki na mtu huyo ataadhibiwa kwa nia yake hii hata kama atakuja kuufanya huu uovu baada ya miaka mingi, na pia yule mwenye kuendelea na kudumu kufanya madhambi madogo madogo basi madhambi hayo yatabadilika na kuwa makubwa, amesema Allah -aliyetukuka-= pindi alipokuwa anataja sifa za waja wema :
{وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَى مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ}
Na hawaendelei na (maovu) waliyoyafanya,na hali wanajua (kuwa hayo ni maovu) .
Aali Imran 135 .
قال العلامة ابن عثيمين -رحمه الله-:
Amesema mwanachuoni mkubwa ibn Uthaimin- Allah amrahamu-:
ولهذا قال العلماء: إن الإصرار على المعصية الصغيرة يجعلها كبيرة؛ لأن إصراره عليها يدل على تهاونه بمن عصاه
Kwa ajili hii wamesema
wanavyuoni :
“ Bila shaka kuendelea kufanya madhambi madogo huyafanya (kuwa) ni makubwa kwa sababu kuendelea kwake juu ya hayo (madhambi) hujulisha juu ya kumdharau yule anayemuasi ”
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tano 9, 1444H ≈ Sep 7, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•