MTU KATIKA TAABIIN ANAYEFANANA MNO NA MTUME -SWALA NA SALAMU ZA ALLAH ZIMFIKIE-

قال ابن الجوزي رحمه الله :

Amesema ibn l-Jauziy -Allah amrahamu-:

« وكان من التابعين رجل يُقال له كابس بن ربيعة السَّامي، من بني سامة بن لؤي، كان يشبههُ [أي: النبي ﷺ ] ،

Na kulikuwa katika taabiin kuna mtu anaitwa Kabis bin Rabi’a Assamiy ni katika ukoo wa Samah bin Luayy ,alikuwa akifanana naye (Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie-)

فبعث إليه معاوية فقبَّل بين عينيه، وأقطعه قطيعة، وكان أنس بن مالك إذا رَآه بكى ! »

basi Muawiyah (aliposikia) akaagiza aletwe (na alipoletwa), akambusu baina ya macho yake na akamkatia kipande cha ardhi, na alikuwa Anas bin Malik pindi anapomuona hulia !

كشف المشكل – لابن الجوزي (١ / ٤٢-٤٣)

Maelezo ya mfasiri:

Wanachuoni wamewataja watu wengi ambao walikuwa wakifanana na Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie- kimaumbile , na kuna riwaya mbalimbali pia zimethibiti katika hilo mfano kauli yake Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- akiielezea nafsi yake katika kisa cha Miiraji -:

(( وأنا أشبهُ ولدِ إبراهيم – عليه السلام – به)).

Na mimi ni mtoto ninaye fanana zaidi na Ibrahimu katika wanaye.

رواه البخاري.

Na katika hao ambao walikuwa wakifanana na Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie- ni huyu Kabis bin Rabia -Allah amrahamu-ambaye alikuwa ni mtu wa Baswrah ,na kumepokewa kuwa watu wa Baswrah walimuandikia Muawiyah-Allah amridhie- walimueleza kuwa , watu wamefitinika na mtu (ambaye) anafanana na Mtume wa Allah -swala na salamu za Allah zimfikie- basi Muawiyah -Allah amridhie-akamuandikia gavana wake wa sehemu hiyo ambaye ni Abdullah bin Kuraiz na akamuamrisha amlete na yeye akampeleka ,basi pindi alipofika kwa Muawiyah -Allah amridhie- , Muawiyah alishuka katika kiti chake cha kifalme na akatembea mpaka mahali alipokuwepo na akambusu baina ya macho yake na akamkatia kipande cha ardhi kama ni takrima yake kwa kule kufanana kwake na Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-.

Tanbih : Attabiun :Ni wale waliokutana na maswahaba hali ni waislamu na wakafa katika uislamu .

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tano 9, 1443H ≈ Sep 7, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *