NASAHA ZENYE THAMANI KWA KILA MWANAFUNZI .

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

NASAHA ZENYE THAMANI KWA KILA MWANAFUNZI !

يا طالب العلم ، لا تقطع نفسك عن هذه الأوراد الأربعة

Ewe mwanafunzi usiizuie nafsi yako na hizi nyiradi nne :

قال الشيخ عبد السلام بن محمد الشويعر -حفظه الله تعالى -:

Amesema sheikh Abdu Salam bin Muhammad Asshuwa’ir -Allah aliyetukuka amuhifadhi-:

١- اجعل لك نصيبا من الدروس لا تقطعها

٢-واجعل لك نصيبا من القرآن لا تقطعه

1-Na jiwekee fungu katika masomo usilikate.

2- Jiwekee fungu katika Quran usilikate .

٣- واجعل لك نصيبا من القراءة لا تقطعه

٤- واجعل لك نصيبا من المذاكرة لا تقطعه

3- Na jiwekee fungu katika kusoma usilikate .

4- Na jiwekee fungu katika mudhakara (kupitia masomo) usilikate .

هذه الأمور الأربعة لا تقطعها قدر استطاعتك ،ومع ذلك أكد عليها بكثرة دعاء الله-عز وجل- أن يرزقك علما نافعا .

Mambo haya manne usiyakate kadri ya uwezo wako , na pamoja na hayo yatilie nguvu hayo (manne) kwa wingi wa kumuomba Allah -aliyeshinda na kutukuka- akuruzuku elimu yenye manufaa.

المصدر :

Ufafanuzi unaotokana na maneno ya sheikh -Allah amuhifadhi- :

Mwanafunzi unatakiwa usiache kutafuta elimu usiizuie nafsi yako na kusoma ,na mwanafunzi anatakiwa awe na uradi wa Qurani ajipangie muda kwa ajili ya kusoma Quran kila siku, na pia awe na uradi wa kutafuta elimu kwa kuhudhuria darasa za wanachuoni na adumu na hili kama alivyoeleza sheikh katika hiki kipande hiki kuwa mmoja katika watu anaowafahamu aliahidiana na sheikh wake kuwa kisiwatenganishe chochote baina yake na sheikh wake isipokuwa kifo , au mmoja wao akishindwa ! , kisha sheikhe akaekeza kuwa yeye anawakumbuka baadhi ya masheikh zamani katika darasa zao walikuwa wakihudhuria wanafunzi wenye umri wa miaka sitini mpaka sabini hawaachi kuhudhuria kwa mwalimu wao , na akaelekeza kuwa anamjua mmoja katika watu yeye huhudhuria darasa la sheikh wake na kusoma kwake na hali ana miaka zaidi ya sitini na tano na alikuwa akihudhuria tokea miaka arobaini mpaka sasa ! na huyu mwanafunzi amefikia daraja kubwa katika elimu kuliko sheikh wake lakini bado anahudhuria kwa sheikh wake !, na hili analolifanya huyu mwanafunzi ni katika unyenyekevu katika elimu na pia kujenga heshima kwa sheikh ,na faida atakayopata huyu mwanafunzi aliyekuwa na unyenyekevu kwa sheikh wake katika kutafuta elimu , ni Allah kuzifanya nyoyo za watu ni zenye kumtukuza mtu huyu na wala hilo haitii mapungufu nafsi yake .

Maelezo ya mwandishi:

Bila shaka hili la mtu kudumu na mwalimu wake ni jambo lenye manufaa mengi kwa mwanafunzi lakini katika zama tulizokuwa nazo ni nadra kuliona bali unaweza ukamuona mwanafunzi anafanya juhudi ya kupekua makosa ya mwalimu wake au kusaidiana na wenye kufanya hivyo, au pengine akamwingiza katika bida’a kabisa na uhizbi ! .

Tunamuomba Allah salama .

Mwandishi : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tano 16, 1443H ≈ Sep 12, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *