FAIDA KATIKA KUAMINI QADARI NA KUSUBIRI JUU YA MABALAA .

كتب الشيخ صالح العصيمي -حفظه الله تعالى- عبر حسابه على تويتر .

Ameandika sheikh Swaleh Al-Uswaim -Allah amuhifadhi- kupitia ukurasa wake wa twitter (maneno yafuatayo) :

لا تدري عمَّا كتب الله من أقداره المؤلمة، فآمن بمكتوبها،

Hauyajui yale aliyoyaandika Allah katika kadari zake zinazoumiza basi yaamini yale yaliyoandikwa ,

وسلِّم بمحتومها، واحمل نفسك على قبولها،

Na jisalimishe kwa yale (ambayo) hakuna budi yatokee na ipeleke nafsi yako katika kuyakubali,

فاشكره عليها، فإن لم تستطع شكره فارضَ بها، فإن لم تستطع الرِّضا بها فاصبر عليها، وذلك أدناها.

Na mshukuru (Allah) juu ya hiyo (mitihani) na Kama haukuweza kumshukuru basi iridhie hiyo (mitihani) na kama haukuweza kuiridhia basi subiri juu ya hiyo (mitihani) na huko (kusubiri) ni (daraja) la chini kabisa.

الأحد ٦ ربيع الأول ١٤٤٤ه‍

Maelezo ya mfasiri:

Mtu anapopatwa na mitihani na mabalaa haepukani na moja wapo katika hali hizi tatu na kama hayupo katika hali hizi basi ataingia katika haramu na sheikh -Allah amuhifadhi-amezitaja hizi hali kwa kuanzia daraja la juu kabisa kiubora na sisi tutazipangilia hivyo hivyo:

1- Daraja la kwanza kwa ubora mtu anapopatwa na mitihani ni kumshukuru Allah -aliyetukuka-katika huo mtihani kama alivyokuwa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-alikuwa anapoona jambo linalomchukiza husema :

” الحمدُ للَّهِ على كلِّ حالٍ “

“ Sifa zote njema ni za Allah juu ya kila hali” .

رواه ابن ماجه والحاكم وغيرهما.

Kwa hiyo hili ni daraja la juu kabisa ambalo muislamu anatakiwa amshukuru Allah -aliyetukuka- shukurani ya kuegemeza mambo yake kwake Allah na kusubiri kwa mabalaa yaliyompata , na kama hatoweza kubaki katika daraja hili basi ashuke chini kidogo .

2- Daraja la pili ni kuridhia ule mtihani uliompata kwa sababu yeye ni kiumbe na ajue kuwa Allah hakadirii shari bali yote yanayowapata waja hata kama kwao ni shari lakini watambue kuwa Allah ameyakadiria kwa hekima maalumu zinazojulika na zisizojulika , na kama ameshindwa kukaa katika daraja hili la kuridhia basi akae katika daraja linalofuata ambalo ni daraja la kusubiri .

3- Daraja la tatu ni kusubiri na daraja hili la kusubiri ni wajibu kwa maana yule asiyeweza kukaa katika daraja hili basi ataporomokea katika daraja la kutoridhia kadari za Allah kwa maana ataingia katika haramu kwa ufupi tunasema hivi mtu anapopatwa na balaa ima ashukuru ima aridhie ima asubiri :

Kushukuru au kuridhia ni sunnah lakini kushukuru ni bora zaidi ya kuridhia,na kusubiri ni wajibu na mja akisubiri na akataraji malipo kutoka kwa Allah basi ana ujira mkubwa mbele ya Allah , na chini ya kusubiri ni kutoridhia kadari na kulalamika jambo ambalo ni haramu kama tulivyoona na Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie-amesema- :

إن عِظَمَ الجزاءِ مع عِظَمِ البلاءِ،

Hakika ukubwa wa malipo (huambatana) na ukubwa wa balaa (mtihani)

وإِنَّ الله -عز وجل – إذا أَحَبَّ قومًا ابتلاهم ؛

na kwa hakika Allah-aliyeshinda na kutukuka- pindi atakapowapenda watu (fulani basi) huwapa mitihani

فمن رَضِيَ فله الرِّضَى، ومن سَخِطَ فله السّخْطُ

basi yule atakayeridhia atapata radhi (za Allah) na atakayechukia atachukiwa (na Allah).

رواه الترمذي .

Hii hadithi ni dalili ya kuwa kusubiri katika mitihani ni wajibu na kuchukia na kukasirika ni haramu na ni katika sababu za kukasirikiwa na Allah na kuadhibiwa huko akhera.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 17, 1444H ≈ Oct 13, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *