MKE ANATAKA NINI ?

قال الشيخ جمال فريحان الحارثي -رحمه الله- :

Amesema sheikh Jamalu Farihan Al-Harithiy -Allah amrahamu-:

« ماذا تريد الزوجة عندما خرجت من بيت والديها إلى عش الزوجية ؟!

“Mke anataka nini pindi alipotoka katika nyumba ya wazazi wake na kuelekea katika makazi (mapya) ya ndoa ?!

  • أكانت ترغب أن تنتقل بين جدران بيت أهلها إلى ما بين جدران بيته ؟

Je alikuwa akipenda kuhama baina ya kuta za nyumba ya familia yake na kuhamia baina ya kuta za nyumba ya huyo (mume) ?

إنها ترغب و بكل صراحة في الدفء و الحنان ، كما ترغب أنت في الهدوء و التمتع مع الزوجة الصالحة ؛

Hakika huyo (mke) anapenda joto (la mapenzi) na huruma kama wewe unavyopenda (kupata) utulivu na kustarehe na mke mwema

فراجع نفسك قبل أن تندم ولات حين مندم »

Basi irejee nafsi yako kabla ya kujuta muda ambao si wakujuta “

🛍 الـــمـــصــدر. 🛍
[الحقوق الزوجية للشيخ جمال الحارثي (ص٤٨)

Maelezo ya mfasiri :

Hizi ni nasaha kwa kila mume aliyeitelekeza familia yake akiwemo mkewe anatakiwa mume ajue kuwa mke naye anahitajia kutoka kwake starehe, mapenzi na huruma na kuishi maisha ya ndoa yaliyokuwa mazuri, na mume anatakiwa ajue kuwa huyo mke hakuacha nyumba ya wazazi wake na akaja kwake kwa ajili ya kubadilisha mazingira ya kuhama kutoka nyumba moja kwenda nyingine ! bali ametoka nyumbani kwake na kuja kwa mume kwa ajili ya kuja kuishi maisha ya ndoa yenye huruma na mapenzi ,kama alivyo mume anayahitajia mambo haya kutoka kwa mke basi na mke naye anahitajia kutoka kwa mume :

Na Allah -Aliyetukuka- amesema:

( وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ )

Na (wanawake) wanayo haki kwa sharia (kufanyiwa na waume zao) kama ile haki iliyo juu yao kuwafanyia waume zao .Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao .

البقرة : ۲۲۸

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 20, 1444H ≈ Oct 16, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *