MWANACHUONI ANAPOKOSEA .

موقفنا إزاء زلة العالم

Msimamo wetu upande wa kosa la mwanachuoni .

قــال الشيخ صالح العصيمي حفظه الله:

Amesema sheikh Swaleh Al-Uswaimiy -Allah amuhifadhi-:

ومما تناسب الإشارة إليه هنا – باختصار وجيز- معرفة الواجب إزاء زلة العالم وهو ستة أمور:

Katika yale yanayonasibiana na kuashiriwa hapa (japo) kwa ufupi sana ni kujua yanayowajibika (kufanywa) upande wa kosa la mwanachuoni nayo ni mambo sita :

الأول: التثبت في صدور الزلة منه.
La kwanza : Kupata uhakika (kwamba) kuna kosa limetoka kwake .

والثاني: التثبت في كونها خطأ، وهذه وظيفة العلماء الراسخين، فيسألون عنها.

Na la pili: Kupata uhakika kuwa hilo (alilofanya) ni kosa na hii ni kazi ya wanavyuoni waliobobea , basi (hao) watamuuliza .

والثالث: ترك اتباعه فيها.

Na la tatu: Kutomfuata katika hilo (kosa) .

والرابع: التماس العذر له بتأويل سائغ.

Na la nne: Kumtafutia udhuru kwa maana inayofaa.

والخامس: بذل النصح له بلطف وسر لا بعنف وتشهير.

Na la tano: Kumpa nasaha kwa upole na kwa siri si kwa ukali na kusambaza .

والسادس: حفظ جنابه فلا تهدر كرامته في قلوب المسلمين.

Na la sita : Kuhifadhi daraja lake na isivunjwe heshima yake katika nyoyo za waislamu .

شرح تعظيم العلم (ص:٩٢).

Maelezo ya mfasiri:

Haya ndiyo yanayowajibika kufanywa pindi mwanachuoni katika wanachuoni wa ahlu Sunnah anapokosea :

1- Kupeleleza na kupata uhakika kuwa hilo kosa limefanywa na yeye.

2- Kuwa na uhakika kuwa hilo alilofanya ni kosa kweli usije ukahukumu kosa na hali si kosa, na kazi hii wataifanya wanavyuoni waliobobea wataenda kumuuliza ili wapate uhakika.

3- Kama itathibiti kuwa amekosea basi haifai kumfuata katika hilo kosa .

4-Kumtafutia udhuru kwa maana inayofaa ,ina maana tumdhanie kheri kuwa huwenda yeye amelifanya hili kuna mahali amekamatia.

5- Kumpa nasaha kwa upole na kwa siri bila ya kumtangaza na kumnanga .

6- Kuhifadhi heshima yake na nafasi yake na kutovunjiwa heshima yake kwa waislamu

Bila shaka haya aliyoyataja sheikh -Allah amuhifadhi-ni katika kuwaheshimu wanavyuoni na masheikh na kuwavunjia adabu wanavyuoni ni katika makosa na madhambi makubwa , Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie – amesema:

“ليس من أمتي – وفي رواية: ليس منا من لم يُجِلَّ كبيرنا، ويَرْحَم صغيرنا، ويعرف لِعَالِمنَا حقَّه”

” Si katika umati wangu -na katika riwaya nyingine: si katika sisi yule asiyemuheshimu mkubwa wetu ,na asiyemuonea huruma mdogo wetu, na asiyejua haki ya mwanachuoni wetu “

(صحيح الجامع: ٥٤٤٣)

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 24, 1444H ≈ Oct 20, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *