موت الشيخ عبد الرحمن بن صالح محي الدين – رحمه الله تعالى
KIFO CHA SHEIKH ABDUL- RRAHMAN BIN SWALEH MUHYI DDIN -ALLAH ALIYETUKUKA AMRAHAMU-.
🎙 قال الحسن- رحمه الله-
AMESEMA AL – HASAN: -ALLAH AMRAHAMU-
”كانوا يقولون : موت العالم ثلمة في الإسلام لا يسدها شيئ ما اختلف الليل والنهار.“
“WALIKUWA WAKISEMA (WEMA WALIOPITA): KIFO CHA MWANACHUONI NI PENGO KATIKA UISLAMU (AMBALO) HALITOZIBWA NA CHOCHOTE MUDA AMBAO USIKU NA MCHANA VINAPISHANA (DUNIA IPO)”
📚 REJEA:- ⇊
أخرجه الدارمي في السنن وابن عبد البر في العلم وأحمد في
الزهد
عن ابن عباس لما دفن زيد بن ثابت حثى عليه التراب ثم قال: هكذا يدفن العلم.
KUTOKA KWA IBN ‘ABBAS PINDI : ALIPOZIKWA ZAIDU BIN THABIT ALIMIMINA UDONGO KWA MIKONO YAKE JUU YA (KABURI),KISHA AKASEMA:
“ HIVI NDIVYO INAVYOZIKWA ELIMU”
📚 REJEA:- ⇊
عبد الرزاق ٦٤٧٩
Maelezo ya mwandishi:
Kifo cha mwanachuoni mmoja ni kama kifo cha umma mkubwa wa watu ,kama alivyosema mshairi:
لعَمْرُكَ ما الرَّزِيَّة فَقْدَ مالٍ *
Naapa kwa umri wako si msiba kukosa mali .
ولا شاةٌ تَمُوتُ ولا بَعِيرُ
Wala mbuzi anayekufa wala ngamia .
ولكنّ الرَّزِيَّة فَقْدُ فذ *
Lakini msiba (haswa) ni kumkosa mtu mmoja
يمُوتُ لِمَوْتِهِ خَلْقٌ كَثِيرُ
(ambaye) hufa kwa kifo chake viumbe wengi .
فنسأل الله أن يرحم الشيخ عبد الرحمن محي الدين رحمة واسعة
“Basi tunamwomba Allah amrehemu sheikh Abdul-Rrahman Muhyi ddin rahma (zilizo) kunjuka .
TANBIH:
Neno ” Naapa kwa umri wako”, ni tamko ambalo lina sura ya kiapo lakini waarabu hawakusudii kiapo .
Mwandishi : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 1, 1444H ≈ Nov 25, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•