KITABU CHA PILI :
9 – Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya aqida /itikadi kwa watoto wa kiislamu .
س رقم: ٩
Swali no.9:
مَا هِيَ مَرَاتِبُ الدِّيْنِ ؟
Ni yepi madaraja ya dini ?
ج:
Jawabu:
مَرَاتِبُ الدِّيْنِ ثَلَاثَةٌ :
الْإِسْلَامُ، وَ الْإِيْمَانُ ، والْإِحْسَانُ .
Madaraja ya dini ni matatu :
Uislamu,na imani,na ihsani/wema .
سلسلة بطاقات: العقيدة لأشبال الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.
[ Mtiririko wa makala za vikadi vya aqidah/itikadi kwa watoto wa kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy Allah amuhifadhi]
Maelezo ya mfasiri:
Mzazi/mlezi hapa atamuelezea mtoto kwa kumwambia :
Mwanangu dini yetu ya kiislamu ina madaraja matatu nayo ni kama yalivyotajwa hapo juu :
1- Uislamu :
Maana ya uislamu hapa ni zile ibada zinazodhihiri kama vile :Swala,zaka ,hija, jihadi, kuamrisha mema na kukataza maovu n.k .
2-Imani:
Maana ya imani hapa ni zile itikadi za moyoni kama vile: Kuamini nguzo sita za imani ambazo tutakuja kuziona katika masomo yetu yanayokuja -inshaallah-
3- Ihsani (Wema) :
Maana ya ihsani/wema ni kuzitengeneza vilivyo itikadi za moyoni na matendo yanayodhihiri, kwa maana kuyafanya yote hayo katika njia ya ukamilifu na ubora .
Usikose makala namba10 inayofuata in shaa Allah
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 26, 1444H ≈ Dec 20, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•