HUYU NDIYE ALIYEIPINDUA DINI YA MASIHI ISA -AMANI IWE JUU YAKE-

قال شيخ الإسلام ابن تيمية رحمه الله تعالى:

Amesema sheikhu l-Islam ibn Taimiyyah -Allah aliyetukuka- amrahamu-

“وقد ذكر أهل العلم أن مبدأ الرفض إنما كان من الزنديق: عبد الله بن سبأ؛ فإنه أظهر الإسلام وأبطن اليهودية، وطلب أن يفسد الإسلام،

Bila shaka wametaja wanavyuoni kwamba mwanzo wa Ushia hakika si vingine ulitokana na mzandiki (mnafiki) Abdullah bin Sabai ,hakika yeye alidhihirisha uislamu na kuficha uyahudi (moyoni) na alitaka kuuharibu uislamu ,

كما فعل بولص النصراني الذي كان يهوديا، في إفساد دين النصارى”

Kama alivyofanya Paul mnaswara ambaye alikuwa myahudi, katika kuiharibu dini ya manaswara

“مجموع الفتاوى” (28/483)

Maelezo ya mtarjumu:

Kama inavyofahamika kuwa asili ya ushia ni uyahudi ulioingizwa na Abdullah bin Sabai ambaye yeye aliingia katika uislamu kwa uwongo lakini moyoni mwake alificha uyahudi kisha baada ya hapo akaanza kudai kuwa aliyestahiki kuwa kiongozi baada ya kufariki Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-ni Aliy bin Abii Twalib -Allah amridhia na madai mengine mbalimbali , na hivi hivi ndivyo alivyofanya Paul mnaswara yeye huyu kipindi ambacho Isa (Yesu) – amani iwe juu yake-yupo alikuwa ni adui mkubwa wa Masih Isa -amani iwe juu yake- lakini baada ya kunyanyuliwa mbinguni tu akajifanya kumkubali Masih na akaanza kulingania lakini mtu huyu alikuwa ni mbaya mno, kwa sababu yeye ndiye aliyeipundua na kuibadili ile dini aliyoifundisha Masih ambayo ni dini waliyoilingania Mitume wote nayo ni dini ya kumuabudia Mungu mmoja ,ambayo ni Uislamu ,basi huyu Paul akafanikiwa kuipindua dini ya Masih -amani imfikie- akaingiza vitu vingi katika dini ya haki kama vile :

1- Itikadi ya msalaba ambayo ni itikadi mama ya dini ya hii ya kinaswara aliyoileta Paul .

2- Itikadi ya utatu ambayo maana yake ni kuwa Mungu ni mmoja katika nafsi tatu .

3-Uungu wa Masih Isa -amani iwe juu yake- wana maanisha kuwa huyo Masihi Isa -amani imfikie- ni Mungu na ndiyo maana utawaona wanamuomba na kumtaka msaada kumuelekea kwa shida zao .

4-Kuamini kuwa Masih ni mtoto wa Mungu -Mwenyezi mungu ametakasika na yote haya wanayoyazusha juu yake-.

Itikadi zote hizi ni itikadi zilizoletwa na huyu Paul na wala hazikufundishwa na Masih- amani imfikie-.

Mwandishi : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 1, 1444H ≈ Dec 25, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *