KITABU CHA PILI :
11 – Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya aqida /itikadi kwa watoto wa kiislamu .
س رقم: ١١
Swali no.11 :
مَا هِيَ أَرْكَانُ الْإِسْلَامِ ؟
Ni zipi nguzo za uislamu ?
ج:
Jawabu:
أَرْكَانُ الْإِسْلَامِ خَمْسَةٌ:
Nguzo za uislamu ni tano :
شَهَادَةُ أَنْ لَّا إِلٰهَ إِلَّا اللّٰهُ ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُوْلُ اللّٰهِ ، وَ إِقَامُ الصَّلَاةِ، وَ إِيْتَاءُ الزَّكَاةُ ، وَ صَوْمُ رَمَضَانَ، وَ حَجُّ الْبَيْتِ .
Kushuhudia kuwa hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allah ,na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allah, na kusimamisha swala, na kutoa zaka ,na kufunga ramadhani, na kuhiji nyumba (tukufu ya Maka)
سلسلة بطاقات: العقيدة لأشبال الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.
[ Mtiririko wa makala za vikadi vya aqidah/itikadi kwa watoto wa kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy Allah amuhifadhi]
Maelezo ya mfasiri:
Mzazi/mlezi hapa atamuelezea mtoto kwa kumwambia :
Mwanangu dini yetu ya kiislamu ina nguzo tano :
Kutokana na umuhimu wa hizi nguzo tano Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie-ameufananisha uislamu ni jengo lililosimama juu ya hizi nguzo tano na mengineyo yasiyokuwa hizi nguzo tano yanazifuata hizi nguzo tano kwa sababu hizi nguzo tano ni msingi, nazo ni kama zifuatazo :
1- Shahada mbili : Hizi shahada mbili ni msingi wa matendo yote na wala ibada haitokubaliwa bila ya kujengeka juu ya hizi shahada mbili , na pia kila moja katika hizi shahada mbili haitimii bila ya mwenzake.
2-Kusimamisha swala: Hii ni nguzo ya pili kwa umuhimu baada ya shahada mbili nayo ni ibada inayofanywa kwa viungo, na ni ibada ya kwanza kuhesabiwa siku ya kiama katika haki za Allah,na ni ibada pekee ambayo Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- amefaradhishiwa akiwa mbinguni .
3- Zaka : Ni ibada ambayo huambatanishwa na swala katika Quran kwa maana pindi inapotajwa swala hutajwa zaka kwa pamoja na zaka ni ibada ya kimali ambayo manufaa yake huenea kwa mtoaji na anayepewa, ama mtoaji hupata thawabu ,na kuzitakasa mali zake na pia anayepewa hunufaika kwa kile anachopewa kwa ajili hii imetangulizwa kutajwa kabla ya funga .
4-Kufunga mwezi wa Ramadhani: Hii ni katika ibada ambazo manufaa yake huishia kwa mfungaji, na ibada hii ni siri baina ya mja na Mola wake kwa sababu muislamu anaweza akawa hakufunga kwa dharura ya kisheria lakini ukimuona huwezi kujua, na lengo kubwa la ibada hii ni kumcha Allah .
5-Kuhiji nyumba tukufu wa Alllah: Hija ni ibada ya kimwili na kimali kwa maana mwenye kuitekeleza ni lazima awe na afya na uwezo wa kuitekeleza kwa sababu ndani yake kuna harakati mbalimbali za kwenda huku na huku , na pia hija inahitaji mali na katika zama zetu tulizokuwepo kuna hitajika passport,viza ,na matumizi yake na kuiachia familia .
Usikose makala namba 12 inayofuata in shaa Allah
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 17, 1444H ≈ Oct 13, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•