KITABU CHA PILI :
13 – Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya aqida /itikadi kwa watoto wa kiislamu .
س رقم: ١٣
Swali no. 13
مَا هِيَ شُرُوْطُ لَا إِلٰهَ إِلَّا اللّٰهُ ؟
Ni zipi sharti za (kushuhudia kuwa) : Hakuna aabudiwaye kwa haki isipokuwa Allah ?
ج:
Jawabu:
شُرُوْطُهَا سَبْعَةٌ :
Sharti zake ni saba:
الْعِلْمُ ، وَالصِّدْقُ ، وَ الْانْقِيَادُ، وَ الْقَبُوْلُ ،والْمَحَبَّةُ، والْإِخْلَاصُ ، والْيَقِيْنُ .
Elimu/kutambua,na ukweli, na kumyenyekea,na kukubali, na kupenda ,na ikhlaswi ,na yakini .
سلسلة بطاقات: العقيدة لأشبال الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.
[ Mtiririko wa makala za vikadi vya aqidah/itikadi kwa watoto wa kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy Allah amuhifadhi]
Maelezo ya mfasiri:
Mzazi /mlezi hapa atamuelezea mtoto kwa kumwambia :
Mwanangu tamko hili la kushuhudia kuwa “hakuna aabudiwaye kwa haki isipokuwa Allah ” lina sharti zake ambazo kama hazijatimia kwa mtu basi uislamu wake haukukamilika ,na idadi yake ni saba kama zilivyotajwa hapo juu, kutokana na umuhimu wake naona tuzifafanue ili upate kuzifahamu vizuri ,ila mwanangu kuwa na subira leo somo letu litarefuka kidogo :
1-Elimu/kujua :
Ni kujua kuwa maana ya tamko hili ni hii : “hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allah” ,na yule mwenye kulitamka tamko hili kwa ulimi na akawa hajui maana yake basi tamko hilo halitomsaidia .
2-Ukweli: Mwenye kulitamka tamko hili awe mkweli, ukweli unaopingana na uwongo,kwa maana unatakiwa moyo wake uafikiane na ulimi wake ,ama yule mwenye kulitamka tamko hili kwa ulimi tu na hali moyo wake unapinga maana ya tamko hili basi mtu huyo ni mnafiki na tamko hili halitomsaidia .
3- Kunyenyekea: Anatakiwa mwenye kutamka tamko hili atekeleze yale yanayojulishwa na tamko hili,kama vile kumpwekesha Allah katika ibada na kutekeleza maamrisho na kuacha makatazo ,ama mwenye kutamka na akaacha kumpwekesha Allah katika ibada basi tamko hili halitomnufaisha.
4- Kukubali : Anatakiwa akubali yote yaliyojulishwa na tamko hili kwa moyo wake na ulimi wake na aamini yote yaliyopo katika uislamu kuwa ni haki na uadilifu , ama yule asiyekubali kuwa anayestahiki kuabudiwa kwa haki ni Allah ,au akaona kuwa dini nyingine isiyokuwa ya kiislamu ni sahihi kama vile wanavyosema baadhi ya wajinga wasiojua kuwa “wanadamu wote tunamuabudia Mungu mmoja isipokuwa tunatofautiana njia tu”, maneno haya ni ukafiri na yeyote mwenye kuamini hivi bila shaka mtu huyo amekufuru, vilevile wale wenye kulingania katika dini mseto bila shaka wanalingania katika ukafiri.
5- Kupenda :Anatakiwa aliyetamka tamko hili alipende na ayapende yale yaliyojulishwa na tamko hili na awapende watu walioshikamana na tamko hili ,ama yule aliyetamka tamko hili lakini akachukia kile kilichojulishwa na tamko hili au akawachukia watu wake kwa sababu ya tauhidi waliyokuwa nayo , yaani wale wanaomuabudia Allah pekee bila ya kumshirikisha na chochote, basi mtu huyo si muislamu
6- Ikhlaswi : Kumtakasia ibada Allah ,kwa maana yule aliyelitamka tamko hili lakini akawa anamshirikisha Allah katika ibada kama walivyo watu wenye kuabudia makaburi ,basi watu hawa na wengine wasioacha ushirikina halitowanufaisha tamko hili kwa sababu katika sharti zake ni kuacha lushirikina .
7- yakini: Hakuna budi kuamini imani ya kukata,kuamini kile kinachojulishwa na tamko hili kuwa hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa ni Allah pekee ,ni lazima awe na elimu ya yakini ama mwenye kuwa na shaka au akadhania tu bila ya kuwa na yakini au akasitasita au akawa hathibitishi kuwa Allah ndiye mwenye kustahiki kuabudiwa pekee na wala havipingi vyenye kuabudiwa kinyume na yeye basi mtu huyo si muislamu .
Usikose makala namba 14 inayofuata in shaa Allah
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 4, 1444H ≈ Dec 28, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•