KITABU CHA PILI :
15- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya aqida /itikadi kwa watoto wa kiislamu .
س رقم: ١٥
Swali no.15 :
مَا هُوَ وَاجِبُ الْمُسْلِمِ تِجَاهَ رَسُوْلِ اللّٰهِ -صلَّى اللّٰهُ عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ ؟
Ni upi wajibu wa muislamu kwa upande wa mtume wa Allah-swala na salamu za Allah zimfikie-?
ج:
Jawabu:
وَاجِبُهُ: أَنْ يُصَدِّقَهُ فِيْمَا أَخْبَرَ ، وَ يُطِيْعَهُ فِيْمَا أَمَرَ، وَ يَجْتَنِب مَا نَهَى عَنْهُ وَ زَجَرَ ، وأن لَّا يُعْبَدَ اللّٰهُ إلَّا بِمَا شَرَعَ
Wajibu wake (muislamu) ni : Kumsadikisha katika yale aliyoyaeleza , na kumtii katika yale aliyoyaamrisha, na kujiweka mbali na yale aliyoyakataza na kuyakemea, na asiabudiwe Allah ila kwa vile alivyoweka katika sheria.
سلسلة بطاقات: العقيدة لأشبال الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.
[ Mtiririko wa makala za vikadi vya aqidah/itikadi kwa watoto wa kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy Allah amuhifadhi]
Maelezo ya mfasiri:
Mzazi/mlezi hapa atamuelezea mtoto kwa kumwambia :
Mwanangu pindi unapotamka na ukaamini kuwa Muhammad -swala na salamu za Allah zimfikie-ni mtume wa Allah kuna mambo kadhaa yanayowajibika kwako, nayo ni hayo yaliyotajwa hapo juu, na mimi nitakufafanulia zaidi, lakini kabla ya kukufafanulia mwanangu unatakiwa ufahamu kuwa mtume wetu -swala na salamu za Allah zimfikie- amekuja na vitu vitatu:
(a) Habari
(b) maamrisho
(c) makatazo
1- Habari alizozieleza Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie- ni wajibu zisadikishwe sawa sawa yawe mambo ya ghaibu kama vile yale yatakayotokea siku ya kiama ,au yatakayotokea kaburini kama vile kuulizwa maswali, au mambo yaliyopita ,au yajayo n.k .
2- Na maamrisho yote aliyoyaamrisha ni wajibu yatiiwe na kutekelezwa .
3-Na yale aliyoyakataza yaachwe kwa maana kila alilolikataza mtume- swala na salamu za Allah zimfikie-basi liachwe .
Na muislamu anatakiwa asiamuabudie Allah -aliyetukuka-isipokuwa kama alivyoelekeza yeye mwenyewe Allah kwa kumfahamisha mtume wake-swala na salamu za Allah zimfikie-,na ibada yoyote ambayo haipo katika sheria na misingi yake basi huo ni uzushi .
Usikose makala namba 16 inayofuata in shaa Allah
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 11, 1444H ≈ Jan 4, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•