KITABU CHA PILI :
16 – Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya aqida /itikadi kwa watoto wa kiislamu .
س رقم: ١٦
Swali no.16 :
مَا هُوَ الْإِيْمَانُ ؟
Imani ni nini ?
ج:
Jawabu:
هُوَ اعْتِقَادُ الْقَلْبِ، وَ نُطْقُ اللِّسَانِ، وَ عَمَلُ الْجَوَارِحِ، يَزِيْدُ بالطَّاعَةِ وَ يَنْقُصُ بالْمَعْصِيَةِ .
Ni kuitikadi kwa moyo, na kutamka kwa ulimi, na kutenda kwa viungo (imani) inazidi kwa twaa na inapungua kwa maasi.
سلسلة بطاقات: العقيدة لأشبال الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.
[ Mtiririko wa makala za vikadi vya aqidah/itikadi kwa watoto wa kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy Allah amuhifadhi]
Maelezo ya mfasiri:
Mzazi/mlezi hapa atamuelezea mtoto kwa kumwambia :
Mwanangu tambua kuwa imani inakusanya vitu hivi vitatu :
1-Kukiri kwa moyo
2- kutamka kwa ulimi
3- Kutenda kwa viungo
Na vilevile tambua kuwa imani inazidi na kupungua ,na bila shaka hili mwanangu linadhihiri kwa mfano huu, watu wawili ambao mmoja wao humtaja Allah -aliyetuka-mara chache na mwingine humtaja mara nyingi bila shaka huyu wa pili imani yake itakuwa imezidi, na vilevile yule mwenye kutekeleza ibada kwa ukamilifu huyu imani yake huongezeka kuliko yule mwenye kutekeleza ibada kwa mapungufu.
Mpaka hapa utakuwa umefahamu mwanangu kuwa pindi muislamu anapokithirisha kufanya ibada basi imani yake huzidi na kuongezeka na pindi anapofanya maasi imani yake hupungua.
Usikose makala namba 17 inayofuata in shaa Allah
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa:☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 19, 1444H ≈ Jan 12, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•