قال العلامة عبد العزيز بن باز رحمه الله:
Amesema mwanachuoni mkubwa Abdul-Aziz bin Baz-Allah amrehemu- :
العناية بالتوبة قبل دخول هذا الشهر الكريم،
Kutilia umuhimu kuleta toba kabla ya kuingia huu mwezi mtukufu (Ramadhani) ,
حتى يدخل عليك وأنت في سلامة من ذنوبك،
ili iingie (Ramadhani) juu yako na hali wewe umesalimika na madhambi yako,
قد محاها الله عنك بالتوبة، ثم العزم الصادق أن تستقيم في رمضان.
Allah ameyafuta hayo (madhambi) yako kwa toba, kisha kuweka maazimio ya kweli ya kuwa na msimamo katika Ramadhani.
📖 [فتاوىٰ نور على الدرب (١٤٩)]
Maelezo ya mfasiri:
Sheikh -Allah amrehemu- anaeleza kuwa inatakiwa kwa muislamu atilie umuhimu kuleta toba kabla ya kuingia mwezi wa ili Ramadhani iingie na hali muislamu ametwaharika na madhambi ,na aweke maazimio ya kweli kuwa ikiingia Ramadhani atakuwa na msimamo kwa kutekeleza yale yaliyowajibishwa juu yake ikiwemo funga ya Ramadhani na suna mbalimbali ikiwemo kisimamo cha tarawehi na kuutafuta usiku wa cheo kwa kufanya ibada .
•┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa : Shabani 28 , 1444H =Mar 20, 2023M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•