UJUMBE KWA WENYE MVI!

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

MWENYE MVI NI KAMA MJA MZITO AMBAYE MIEZI YAKE YA KUJIFUNGUA IMETIMIA !

‏ قال ابن رجب الحنبلي – رحمه الله:

Amesema ibn Rajab Al-hanbaliy -Allah amrahamu-:

من نزل به الشيب فهو بمنزلة الحامل التي تمت شهور حملها فما تنتظر إلا الولادة ،

Yeyote aliyetokwa na mvi basi huyo ni kama mja mzito ambaye miezi yake (ya kujifungua) imetimia hakuna anachosubiri isipokuwa kujifungua,

كذلك صاحب الشيب لا ينتظر إلا الموت ، فقبيح منه الإصرار على الذنب  .!

Vilevile mwenye mvi hakuna anachosubiri isipokuwa kifo, basi ni vibaya kwake kuendelea na madhambi !

‌‌‌‌‌⤶ لطائف المعارف (٣٤٦/١) .

Maelezo ya mfasiri:

Bila shaka aghlabu mvi ni alama ya mtu kufikia utu uzima na mtu anapofikia utu mzima anatakiwa ajiandae na kukutana na Mola wake kwa sababu umefika muda wake wa kuondoka duniani ,ama kama mtu akifikia umri huo na bado akawa anaendelea na maovu na machafu basi hiyo ni alama mbaya kwake ,na yamethibiti maneno kutoka kwa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- amesema :

” أَعْذَرَ اللَّهُ إِلَى امْرِئٍ أَخَّرَ أَجَلَهُ حَتَّى بَلَّغَهُ سِتِّينَ سَنَةً”

“ Allah ameondoa udhuru kwa mtu aliyemrefushia umri wake mpaka akamfikisha miaka sitini”

رواه البخاري

Kwa maana mtu aliyefikisha umri wa miaka sitini (60) basi huyo hana udhuru mbele ya Allah kwa sababu amefikia umri ambao hakuna kilichobakia kwake isipokuwa ni kurudi kwa Allah kwa kukithirisha ibada na twaa kwa sababu kifo kinakaribia kwake.

Na kutokwa na mvi ni miongoni mwa waonyaji ambao wametajwa na Allah pale aliposema :

{ أَوَلَمۡ نُعَمِّرۡكُم مَّا یَتَذَكَّرُ فِیهِ مَن تَذَكَّرَ وَجَاۤءَكُمُ ٱلنَّذِیرُۖ فَذُوقُوا۟ فَمَا لِلظَّـٰلِمِینَ مِن نَّصِیرٍ }

“ Kwani hatukukupeni umri wa (kuweza) kukumbuka mwenye kukumbuka ? Na akakujieni muonyaji .Basi onjeni (adhabu) madhalimu hawana wa kuwanusuru”

فاطر ٣٦-٣٧

Hapo wataambiwa hao makafiri siku ya kiama kuwa walijiwa na muonyaji, na baadhi ya wafasiri wamesema kuwa muonyaji hapa ni mvi kwa hiyo ndugu yangu unapotokwa na mvi basi tambua kuwa unaonywa kuwa kifo kinakaribia kwako !

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 13, 1444H ≈ Sep29, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *