Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
كتب الشيخ صالح العصيمي -حفظه الله تعالى- عبر حسابه على تويتر .
Ameandika sheikh Swaleh Al-Uswaim -Allah amuhifadhi- kupitia ukurasa wake wa twitter (maneno yafuatayo) :
اسْتِواءُ الْبَاطِنِ والظَّاهِرِ، والسَّلامةُ مِنَ التَّلوُّنِ والنِّفاقِ:
Kulingana sawa kwa moyo na dhahiri, na kusalimika kutokana na kubadilika badilika na unafiki
صفةُ صحيح الدِّين، شُجاعِ الْقَلْبِ، وبها يكون سعيدًا مطمئنًا، فتزيَّنوا بها تنعموا.
(hiyo ni) sifa ya mwenye dini sahihi, shujaa wa moyo , na kwa (tabia) hiyo atakuwa ni mwenye raha na utulivu, basi jipambeni na (sifa) hizo mutaneemeka .
السبت ١٧ صفر ١٤٤٥ه
Maelezo ya mfasiri:
Muislamu anatakiwa awe hivi yaani moyo wake na muonekano wake vyote viwe sawa ,anachokitamka kwa ulimi wake ndicho hichohicho kinatakiwa kiwe moyoni mwake maadamu ni haki, na wala asiwe na tabia ya kinafiki akadhihirisha kinyume na yale yaliyopo moyoni mwake kwa ajili ya maslahi fulani au kumuogopa mtu fulani, na wala asiwe ni mwenye kubadilika badilika kama kinyonga, ukiwa utajipamba na tabia hii yakawa yale yaliyopo moyoni mwako yanaafikiana na muonekano wako basi hiyo ni sifa ya mtu mwenye dini sahihi na shujaa wa moyo ,na kwa sifa hiyo utakuwa na raha na mwenye utulivu, na mwisho sheikh akawahimiza watu wajipambe na sifa hiyo .
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 26, 1445H ≈ Oct 11, 2023M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•