MANHAJI (NJIA) YA SHEIKH IBN BAZ-ALLAH AMRAHAMU- KATIKA KUMKOSOA ALIYEENDA KINYUME NA SHERIA!

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

منهج الشيخ العلامة عبد العزيز بن باز -رحمه الله – في الرد على المخالفين .

Manhaji (njia) ya sheikh ,mwanachuoni mkubwa Abdul-Aziz bin Baz -Allah amrehemu -katika kuwakosoa walioenda kinyume na haki .

قال الشيخ سالم الطويل -حفظه الله- :

Amesema sheikh Salim Attwawil-Allah amuhifadhi-:

يصف لنا أحد ابرز طلاب الشيخ ابن باز رحمه الله تعالى ونائبه في رئاسة الجامعة الإسلامية في المدينة وهو الشيخ المحدث الفقيه عبد المحسن العباد البدر حفظه الله،

Anatuelezea mmoja katika wanafunzi waliodhihiri zaidi wa sheikh ibn Baz -Allah amrahamu- na (alikuwa) naibu wake katika uongozi wa chuo kikuu cha kiislamu cha Madina naye ni sheikh mwanachuoni wa hadithi mjuzi wa fiqih, Abdul-Muhsin Al-bbad Al-badr -Allah amuhifadhi-,

أقول يصف منهج الشيخ ابن باز رحمه الله في الرد على المخالفين فيقول:

Nasema (hivi) akielezea namna (ilivyokuwa) manhaji (njia) ya sheikh ibn Baz -Allah amrahamu-katika kuwakosoa wale walioenda kinyume na njia ya sawa :

هو منهج يتسم بالرفق والشفقة والحرص على سلامة المردود عليه ورجوعه إلى الصواب.

Ni njia (manhaji) inayopambanuka kwa upole na huruma na (kuwa na) pupa juu ya usalama wa anayekosolewa na (kupenda kwake) arejee katika haki.

ومن منهجه أيضا – رحمه الله – أنه إذا رد على مخالف لم يشغل نفسه بمتابعته، ولم يهجره أو يدعو إلى هجره،

Na katika manhaji (njia) yake pia -Allah amrahamu-kwamba yeye anapomkosoa (huyo) aliyeenda kinyume na haki, haishughulishi nafsi yake kwa kumfuatilia ,na (pia huwa) hamuhami na wala hawalinganii (wengine) wamuhame

بل اعتبر نفسه أدى ما عليه من النصح وبيان الخطأ

Bali huizingatia nafsi yake kuwa ametekeleza lile linalowajibika juu yake katika kutoa nasaha na kubainisha kosa

واشتغل بما هو ديدنه من العلم والعمل والدعوة إلى الخير ونفع الناس بمختلف وجوه النفع

Na hushughulika na yale ambayo ni kawaida yake ambayo ni kufundisha na ibada na kuwalingania watu katika heri na kuwanufaisha watu kwa njia mbalimbali za heri .

انتهى كلامه من مقدمة كتاب منهج الشيخ عبدالعزيز بن باز في الرد على المخالفين لنايف بن ممدوح.

Yameisha maneno yake (sheikh) -Allah amrahamu- kutoka utangulizi wa kitabu:

Manhaj ya sheikh, Abdul-Aziz bin Baz – katika kuwakosoa walioenda kinyume na haki (kitabu) cha Nayif Mamduh .

فأقول: فيا ليتنا نسلك منهج الشيخ العلامة والد العلماء والعامة عبدالعزيز بن باز رحمه الله تعالى

فإن ردوده محفوظة مطبوعة مفيدة نافعة جامعة.

(Kisha sheikh Salim Attwawil -Allah amuhifadhi- akasema hivi) :

Basi nasema (hivi) : Ee ! lau sisi tungefuata njia ya sheikh , mwanachuoni mkubwa mzazi wa wanavyuoni na watu wa kawaida Abdul-Aziz bin Baz -Allah aliyetukuka amrahamu- na bila shaka radi zake zimehifadhiwa ,(na) zimechapwa na ni zenye kuleta faida (tena) faida iliyokusanya .

Maelezo ya mfasiri :

Naapa kwa Allah lau watu tungekuwa kama walivyokuwa wanachuoni wakubwa na mfano wa hao ni Sheikh ibn Baz -Allah amrahamu- huyu ni miongoni mwa masheikh ambao Allah alimruzuku elimu ,huruma ,upole na tabia njema kwa ujumla na tunamshukuru Allah tumesimuliwa mengi kutoka kwa masheikh zetu waliomdiriki shekhe huyu , na hiyo ndiyo manhaji yake sheikh -Allah amrahamu- katika kuwakosoa wale waliokosea kinyume na watu wengi katika zama hizi, na manhaji ya sheikh anaieleza mwanafunzi wake mkubwa mwamba katika miamba ya elimu ya hadithi iliyobakia .

Tanbih :

Kuna ndugu zetu Allah -awaongoze – ukimtaja sheikh Abbad -Allah amuhifadhi- utawasikia wakisema :

“Sheikh yeye hapigi radi ndiyo maana darsa yake wanahudhuria hata mahizb! ”, na maneno haya nimeyasikia kwa sikio langu kutoka kwa baadhi ya ndugu zetu !

Sisi hatuna lakusema isipokuwa tunasema hivi :

Allah awaongoze ndugu zetu hawa .

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo pili 23, 1445H ≈ Oct 11, 2023M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *