MWANAMUME NI HUYU !

   عن عبيد بن أمّ كلاب أنّه سمع عُمَر بنُ الخطّاب رضي الله عنه وهو يخطب الناس وهو يقول :

Kutoka kwa ‘Ubaid bin Umm Kilab kwamba yeye alimsikia Umar bin Al-khattwab- Allah amridhie- hali akiwahutubia watu :

” لا يعجبنّكم مِنَ الرَّجُل طَنْطَنَتُهُ وَ لَكِنَّهُ مَنْ أَدَّى الأَمَانَة ، وَ كَفَّ عَنْ أَعْرَاضِ النَّاس فَهُوَ الرَّجُل “.

” Yasikupendezesheni kutoka kwa mtu maneno yake ,lakini hakika hali ilivyo yule mwenye kutekeleza amana ,na akajizuia na (kuchafua) heshima za watu basi huyo ndiye mwanamume”

📚الزهد لابن المبارك ٢٩٥.

🖇 قال الشيخ عبد الرزاق البدر حفظه الله :

Amesema sheikh Abdul-Rrazzaq Al-badr -Allah amuhifadhi-:

أي لا تغترّ بتزيين الرّجل حديثه و تزويقه كلامه ،

Maana yake: Usihadaike na mtu kuyapamba mazungumzo yake na kuyaremba maneno yake

فالرجولة حقًّا في أداء الأمانة و عدم إضاعتها ،

Uwanamume wa kweli ni kutekeleza amana na kutoipoteza hiyo (amana)

و في الكفّ عن أعراض النّاس و عدم اقتراضها.

na katika kujizuia (kuchafua)  heshima za watu na kutowasengenya .

Maelezo ya mfasiri:

Huyu ndiye mwanamume wa sawa sawa, ambaye amekusanya sifa hizi :

1- Mwenye kutekeleza amana, maana yake : Ni mwenye kutekeleza yote ambayo yanawajibika juu yake.

2- Mwenye kuuzuia ulimi wake na mikono yake na kuwaudhi waislamu na watu wote kwa ujumla kama vile :Kuwasengenya, kuwazushia n.k,

Mfasiri : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imerudiwa :Mfungo pili 14, 1443H ≈ Jun 14, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

         •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *